Chanzo cha picha, BBCNEWS
Dakika 18 zilizopita
Nini kinatokea wakati mtu tajiri zaidi na mwanasiasa mwenye nguvu zaidi duniani wanashikana mashati?
Ulimwengu unagundua - na sio picha nzuri. Donald Trump na Elon Musk wana megaphone mbili kubwa zaidi, na sasa wamezielekeza kwa kila mmoja wao, kwasababu kutoelewana kwao kumesababisha vita vikubwa vya maneno.
Trump ametishia shughuli kubwa za kibiashara za Musk na serikali ya shirikisho, ambayo ni msingi wa mpango wake wa SpaceX.
"Njia rahisi zaidi ya kuokoa pesa katika bajeti yetu, mabilioni na mabilioni ya dola, ni kusitisha ruzuku na kandarasi za kiserikali za Elon," Trump alichapisha kwa vitisho kwenye tovuti yake ya mtandao wa kijamii.
Ikiwa Trump atageuza mifumo ya serikali dhidi ya Musk, bilionea huyo wa teknolojia atahisi uchungu. Bei ya hisa ya Tesla ilishuka kwa 14% Alhamisi.
Sio barabara ya njia moja, hata hivyo. Baada ya matamshi hayo, Musk alitoa wito wa kushtakiwa kwa Trump na akathubutu kupunguza ufadhili wa kampuni zake.
Musk pia alisema alikuwa akiharakisha uondoaji wa chombo chake cha anga cha Dragon, ambacho Marekani inakitegemea kubeba wanaanga na vifaa vya Marekani hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.
Lakini saa chache baadaye, alionekana kurudi nyuma kutokana na tishio hilo, akisema akijibu chapisho kwenye X lililomtaka atulie: "Ushauri mzuri. Sawa, hatutamkatalia Dragon."
Musk ana rasilimali zisizo na kikomo za kujibu, ikiwa ni pamoja na kufadhili wapinzani wa Republican katika uchaguzi na mchujo wa mwaka ujao.
Na Alhamisi alasiri, alisema atatoa "bomu kubwa sana" - akipendekeza bila ushahidi kwamba Trump anaonekana kwenye faili ambazo hazijatolewa zinazohusiana na mshukiwa wa ngono marehemu Jeffrey Epstein.
Katibu wake wa vyombo vya habari, Karoline Leavitt, alitoa msukumo wa hasira kwa madai na shutuma za Musk.
"Hiki ni kipindi cha bahati mbaya kutoka kwa Elon, ambaye hajafurahishwa na Muswada wa One Big Beautiful kwa sababu haujumuishi sera alizotaka," alisema.
Musk anaweza asishinde vita dhidi ya serikali yote ya Trump, lakini anaweza kumweka Trump na Republicans katika hali mbaya ya kifedha , kisiasa na ya kibinafsi.
Trump, labda akijua hili, alionekana kupunguza joto kidogo mwishoni mwa siku.
Aliepuka kutoa maoni yake kuhusu Musk wakati wa kuonekana hadharani kwenye hafla ya Ikulu ya White House na akachapisha ujumbe kwenye mtandao wa Truth Social ambao ulisema kwamba hajali "kumgeuka", lakini anatamani angeacha utumishi wa serikali miezi kadhaa iliyopita.
Kisha alijitolea kuongeza sheria yake "kubwa, nzuri" ya ushuru na matumizi.
Pia unaweza kusomaBiashara ya matusi na vitisho
Ugomvi huo ulianza kwa kasi wiki iliyopita, ulianza kutokota Jumatano na kuwa jipu kamili Alhamisi alasiri katika Ofisi ya Oval.
Wakati Kansela mpya wa Ujerumani Friedrich Merz - mgeni wa siku hiyo - aliketi katika ukimya usio wa kawaida, rais alionekana kama mpenzi aliyepuuzwa.
Alionyesha kushangazwa na ukosoaji wa Musk wa sheria yake. Alirudi nyuma dhidi ya dhana kwamba angeshindwa katika uchaguzi wa rais wa mwaka jana bila Musk mamia ya mamilioni ya dola kumuunga mkono.
Na alisema Musk alikuwa akibadilisha tu sauti yake sasa kwa sababu kampuni yake ya gari, Tesla, itaumizwa na msukumo wa Republican kukomesha mikopo ya ushuru wa gari la umeme.
Chanzo cha picha, Trump/Truth and social
Musk aliingia haraka kwenye akaunti yale ya kijamii, X, kwa wafuasi wake milioni 220 na kujibu : "Sijali".
Alisema hajali ruzuku ya magari, na kwamba anataka kupunguza deni la taifa, ambalo anasema ni tishio kwa taifa.
Alisisitiza kuwa Democrats wangeshinda katika uchaguzi wa mwaka jana bila msaada wake. "Huna shukrani," alimwambia Trump.
Bilionea huyo kisha alianzisha mfululizo wa mashambulizi ya ajabu mchana kutwa, na ugomvi ulikuwa mkali.
Chanzo cha picha, elon/x
Musk na Trump walikuwa wameunda muungano wenye nguvu lakini ambao haukutarajiwa, uliishia kwa bilionea huyo wa teknolojia kuwa na nafasi muhimu ya mamlaka ya kupunguza bajeti katika utawala wa Trump.
Idara ya Musk ya Ufanisi wa Serikali, au Doge, ikawa moja ya hadithi kubwa zaidi ya siku 100 za kwanza za Trump, kwani ilifunga mashirika yote na kufukuza maelfu ya wafanyikazi wa serikali.
Haikuchukua muda, hata hivyo, kabla ya uvumi kuanza juu ya lini - na vipi - watu hao wawili wakubwa hatimaye wangeachana.
Kwa muda, ilionekana kama utabiri huo usingetokea. Trump alisimama upande wa Musk hata umaarufu wa Musk uliposhuka, huku akizozana na maafisa wa utawala na alipokuwa mwajibikaji katika chaguzi kadhaa muhimu mapema mwaka huu.
Kila wakati ilipoonekana kungekuwa na mapumziko, Musk angetokea katika Ofisi ya Oval, au chumba cha Baraza la Mawaziri au kwenye ndege ya rais ya Air Force One kuelekea Mar-a-Lago.
Wakati siku 130 za Musk kama "mfanyikazi maalum wa serikali" zilimalizika wiki iliyopita, wawili hao walitumwa kwa ofisi ya Oval, na ufunguo wa dhahabu wa Ikulu ya White House na vidokezo kwamba Musk anaweza kurudi siku moja.
Ni salama kusema kwamba mwaliko wowote umeghairiwa na kufuli zimebadilishwa.
"Mimi na Elon tulikuwa na uhusiano mzuri," Trump alisema Alhamisi - maoni maarufu kwa matumizi yake ya wakati uliopita.
Kumekuwa na mawazo kwamba tangazo la mshangao la Trump mnamo Jumatano usiku la marufuku mpya ya kusafiri, vikwazo vya ziada kwa Harvard na uchunguzi wa njama wa utawala wa Rais wa zamani Joe Biden zote zilikuwa juhudi za kubadilisha mada kutoka kwa ukosoaji wa Musk.
Ikulu ya White House na washirika wake katika Congress walionekana kuwa waangalifu kutomkasirisha zaidi baada ya maoni yake ya hapo awali.
Kisha Trump alizungumza na ... sana kwa hilo.
Mchezo wa pata potea
Sasa swali ni wapi mzozo utaelekezwa. Warepublican wa Congress wanaweza kupata ugumu wa kuunga mkono mswada wa Trump huku Musk akitoa kejeli na, labda ya kifedha, kwa wale wanaovunja safu.
Trump tayari ametishia kandarasi za serikali ya Musk, lakini pia anaweza kulenga washirika wake waliobaki wa Doge katika utawala au kufungua tena uchunguzi wa enzi ya Biden kuhusu biashara ya Musk.
Kila kitu katika hatua hii kiko kwenye meza.
Wakati huo huo, Wanademokrasia wako kando, wanashangaa jinsi ya kujibu. Wachache wanaonekana kuwa tayari kumkaribisha Musk, mfadhili wa zamani wa chama chao, kurudi kwenye kundi.
Lakini pia kuna msemo wa zamani kwamba adui wa adui ni rafiki.
"Ni mchezo wa sifuri," Liam Kerr, mwanamkakati wa Kidemokrasia, aliiambia Politico. "Chochote anachofanya ambacho kinaelekea zaidi kwa Democrats kinaumiza Republican."
Angalau, Wanademokrasia wanaonekana kuwa na furaha kusimama nyuma na kuwaruhusu watu hao wawili kupigana makofi.
Na hadi watakapoachana na vita hivi, mgogoro huu unaweza kuzima kila kitu kingine katika siasa za Marekan
Lakini usitarajie ugomvi huu kuisha hivi karibuni.
"Trump amebakiza miaka 3.5 kama rais," Musk aliandika kwenye X, "lakini nitakuwepo kwa miaka 40-plus."
Pia unaweza kusomaImetafsiriwa na Seif Abdalla