Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Charlotte Coates
- Nafasi, BBC
Dakika 15 zilizopita
Mshambuliaji chipukizi wa Barcelona, Lamine Yamal anaweza kugharimu takriban pauni milioni 340 ikiwa unataka kumnunua, kulingana na kituo cha utafiti cha Uswizi, ambacho hutathmini thamani ya wachezaji mahiri.
CIES Football Observatory, imepiga mahesabu kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 ambapo ni euro milioni 400 (£340m) - karibu mara mbili ya thamani ya uhamisho ulioweka rekodi ya dunia wa Neymar wa euro milioni 222 kutoka Barcelona hadi Paris St-Germain 2017.
Kinda huyo wa Uhispania ni mchezaji wa tano mwenye umri mdogo kucheza mechi yake ya kwanza ya La Liga akiwa na umri wa miaka 15 na miezi tisa.
Amefunga mabao 23 ambayo ni mengi zaidi kuliko mshindi wa Ballon d'Or mara nane Lionel Messi akiwa na umri huo huo.
Yamal alihusika katika mafanikio ya Uhispania ya Euro 2024 - akawa mchezaji bora chipukizi katika mashindano hayo - na pia kubeba mataji mawili ya La Liga na Copa del Rey akiwa na Barcelona.
Alishinda tuzo ya mwaka jana ya Golden Boy, inayotolewa kwa mchezaji bora wa Ulaya chini ya miaka 21.
Mkataba wa miaka sita aliosaini na klabu hiyo ya Catalan wiki iliyopita unajumuisha kipengele cha kulipa euro bilioni moja ili kuvunja mkataba huo kwa klabu inayotaka kumnunua.
Pia unaweza kusomaTano Bora
Yamal, ambaye anatimiza umri wa miaka 18 mwezi Julai, amemzidi mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland, 24 kwa thamani ya pauni milioni 140 zaidi – Haalnd yuko katika nafasi ya pili kwa thamani ya euro milioni 240 (sawa na pauni milioni 200)
Mshambulizi wa Real Madrid, Jude Bellingham ndiye mchezaji mwenye thamani zaidi kutoka Uingereza kwenye orodha hiyo akiwa na thamani ya euro milioni 234 (£197m) huku mchezaji mwenzake Kylian Mbappe akiwa na thamani ya euro milioni 193 (£162m).
Aliyeingia kwenye tano bora ni fowadi wa Bayern Munich na Ujerumani Jamal Musiala, mwenye thamani ya euro milioni 155m (£130m).
Wachezaji 10 wenye thamani zaidi
1 Lamine Yamal (Barcelona) £340m.
2 Erling Haaland (Man City) £200m.
3 Jude Bellingham (Real Madrid) £197m.
4 Kylian Mbappe (Real Madrid) £162m.
5 Jamal Musiala (Bayern Munich) £130m.
6 Pedri (Barcelona) £121m.
7 Vinicius Junior (Real Madrid) £109.7m.
8 Cole Palmer (Chelsea) £106.5m.
9 Julian Alvarez (Atletico Madrid) £106m.
10 Florian Wirtz (Bayer Leverkusen) £103m.
Beki mwenye thamani ya juu zaidi kwenye orodha hiyo ni chipukizi wa Barcelona, Pau Cubarsi, thamani ya euro milioni 118 (£99m) huku Bart Verbruggen wa Brighton akiorodheshwa kama golikipa mwenye thamani ya ya juu zaidi ya euro milioni 64 (£54m).
Mchezaji wa 10 kwenye orodha hiyo kiungo mshambuliaji wa Ujerumani, Florian Wirtz, ambaye anatarajiwa kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza Liverpool kwa kile kinachotarajiwa ununuzi mkubwa katika soka la Uingereza.