Chanzo cha picha, Getty Images
Dakika 5 zilizopita
Newcastle wanamfuatilia Anthony Elanga wa Nottingham Forest, Arsenal wanavutiwa na Benjamin Sesko huku Manchester United ikitoa ofa bora zaidi kwa Bryan Mbeumo.
Newcastle United wamefanya mpango wa kujaribu kumsajili winga wa Uswidi Anthony Elanga, 23, kutoka Nottingham Forest. (Mail)
Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wamewasilisha ofa nyingine ya £100m pamoja na nyongeza ya £13m kwa kiungo wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz, lakini klabu hiyo ya Bundesliga bado inataka zaidi ili kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22. (Mail)
Arsenal wamewasiliana na RB Leipzig kumsajili mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 22, ingawa bado hakuna ofa iliyowasilishwa. (Sky Sports)
Pia unaweza kusoma:Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wametoa ofa yenye thamani ya £60m kwa winga wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, 25, baada ya ofa yao ya kwanza ya jumla ya pauni milioni 55 kukataliwa. (ESPN)
Inter Milan wamefanya mawasiliano rasmi kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Denmark mwenye thamani ya pauni milioni 40 Rasmus Hojlund, 22. (Telegraph - subscription required)
Chanzo cha picha, Getty Images
Lyon wamekataa ofa ya kwanza ya Manchester City kwa kiungo mshambuliaji wa Ufaransa Rayan Cherki, 21, huku mazungumzo kati ya klabu hizo mbili yakiendelea. (Florian Plettenberg)
Tottenham italazimika kulipa zaidi ya pauni milioni 10 iwapo wanataka kumleta kocha wa Brentford Thomas Frank kuchukua nafasi ya Ange Postecoglou, ambaye ametimuliwa na Spurs. (Mirror)
Chanzo cha picha, Getty Images
Mabingwa wa Serie A Napoli wanafikiria kumnunua mlinzi wa Uingereza Trevoh Chalobah, 25, ambaye aliisaidia Chelsea kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa na kushinda Uefa Conference League baada ya kurejea kutoka kwa mkopo Crystal Palace mnamo mwezi Januari. (Telegraph - subscription required)
Bayern Munich, Real Madrid na AC Milan wanamfuatilia kwa karibu mlinda lango wa Italia Gianluigi Donnarumma, 26, ikiwa atashindwa kuafiki mkataba mpya katika klabu ya Paris St-Germain, huku Inter Milan na Juventus wakisubiri mkataba wake umalizike 2026. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazomtaka mlinda mlango wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 30, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 5 katika mkataba wake Chelsea. (Evening Standard)
Kiungo wa kati wa Uingereza Angel Gomes, ambaye anatazamiwa kuondoka Lille mwishoni mwa mkataba wake msimu huu wa joto, ana makubaliano ya kujiunga na Marseille, ambao wamewashinda Tottenham na West Ham kumchukua mchezaji huyo wa miaka 24. (RMC Sport - in French)
Marseille wametoa ofa ya mkataba kwa beki wa West Ham na Morocco, Nayef Aguerd, 29. (Foot Mercato - in French)
Chanzo cha picha, Getty Images
Crystal Palace wanatafuta dili kubwa kwa mlinzi wa Sporting na Ivory Coast Ousmane Diomande, ambaye atawagharimu takriban £45m. (Telegraph - subscription required)
Newcastle wanazidi kuchanganyikiwa kutokana na ada za uhamisho za juu huku bei ya mchezaji wa Eintracht Frankfurt ya pauni milioni 80, Hugo Ekitike ikiwatoa morali Magpies kumnunua mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22. (Telegraph - subscription required)
Chanzo cha picha, Rex Features
Sunderland wamekataa ofa kutoka kwa Borussia Dortmund kwa kiungo wa kati wa Uingereza Jobe Bellingham, lakini vilabu hivyo bado vipo kwenye mazungumzo kuhusu mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19. (Sky Sports Germany)
AC Milan wameonyesha nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen wa Uswizi Granit Xhaka, 32, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikionekana kutaka kumnunua beki wa Ujerumani Malick Thiaw, 23, kutoka klabu hiyo ya Serie A. (Kicker - in German)