Chanzo cha picha, Maxar
Dakika 52 zilizopita
Picha mpya za satelaiti za kituo cha anga cha Belaya cha Urusi katika eneo la Irkutsk zinaonyesha matokeo ya uvamizi wa ndege zisizo na rubani za Ukraine.
Uwanja huo wa ndege ulishambuliwa tarehe mosi mwezi Juni.
Ndege hizo zisizo na rubani pia zililenga kituo cha anga cha Olenya katika eneo la Murmansk.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imethibitisha kushambulia vituo vitano vya anga na tayari rais Vladimir Putin ameonya kulipiza kisasi.
Kulingana na ripoti yake, shambulio hilo la viwanja vya ndege katika mikoa ya Ivanovo, Ryazan na Amur haukufanikiwa, na katika mikoa ya Murmansk na Irkutsk ulisababisha moto katika "vitengo kadhaa vya vifaa vya anga."
Kulingana na picha za hivi karibuni, ndege za kivita za kimkakati za Urusi Tu-95, ziliharibiwa kwenye uwanja wa ndege wa Belaya.
Picha hizo pia zinaonyesha ndege nne zilizoharibiwa, pengine ndege za masafa marefu za Tu-22M3.
Siku ya Jumatatu, mchambuzi wa OSINT Chris Bigers alichapisha picha za satelaiti za rada za uwanja wa ndege wa Belaya, ambazo alizichunguza na kupendekeza kuwa ndege nynegine aina ya Tu-95 huenda pia iliharibiwa .
Katika picha zilizopigwa mnamo Juni 4, kuna ndege ilosalia katika eneo moja, ingawa hakuna dalili za uharibifu zilizoonekana .
Picha hizo pia zinaonyesha ndege nne aina ya Tu -22M3 zilizoharibiwa. ambazo zinawiana na tathmini za awali zilizofanywa na watafiti wa OSINT asubuhi baada ya uvamizi huo.
Idhaa ya BBC Urusi ilichapisha picha mpya za kituo cha ndege, kilichokuwa na ndege hizo kabla ya uvamizi huo.
Picha hii inaonyesha sehemu ya kuegesha ndege aina ya Tu-95. Ndege tatu ziliharibiwa katika eneo hilo.
Pia unaweza kusomaPicha inayofuata inaonyesha sehemu ya kuegesha ndege za mashambulizi ya masafa marefu za Tu-22M3, moja ambayo iliteketea.
Kumbuka kuwa maeneo ambayo ndege zimeegeshwa yamezingirwa na ngome za udongo ili kulinda dhidi ya uchafu unaoruka endapo kuna shambulio la uwanja wa ndege.
Picha nyingine kutoka kwa Tu-22M3. Ndege mbili zimeharibiwa. Madoa meusi ya nyasi zilizoungua yanaonekana karibu na maeneo ya maegesho ya ndege.
Picha hizi zonaonyesha ndege aina ya Tu-22M3 iliyochomwa - ilikuwa ya mwisho katika safu ya ndege kama hiyo.
Kambi ya kijeshi ya 'Olenya'
Ndege pia ziliharibiwa katika uwanja wa ndege wa Olenya katika mkoa wa Murmansk.
Ndege aina ya Tu-22M3 zimekuwa zikiegeshwa katika kambi hiyo. Lakini muda mfupi kabla ya shambulio la Olenya, ripoti ambazo hazijathibitishwa ziliibuka kwamba kamandi ya Urusi ilihamisha ndege za kimkakati za anga kutoka kwa uwanja mwingine wa ndege, Engels-2 katika mkoa wa Saratov.
Uwanja wa ndege wa Saratov tayari umekuwa shabaha ya mashambulizi ya UAVs ya Ukraine mara kadhaa; wachambuzi wa mitandao ya kijamii walieleza uamuzi wa kuhamishia ndege hizoo kwenye rasi ya Kola kwa nia ya kuzilinda na mashambulizi ya angani.
Siku ya Jumapili, video zilizochukuliwa na ndege zisizo na rubani zikishambulia ndege aina ya Tu-95 zilionekana kwenye mtandao.
Chaneli ya uchanganuzi ya OSINT OSINTtechnical ilichapisha rekodi hizi, na kuziita mashambulizi kwenye uwanja wa ndege wa Olenya. Chaneli nyingine, AviVector, ambayo ni mtaalamu wa kuchambua picha za satelaiti za viwanja vya ndege, ilithibitisha kuwa video hiyo inaonyesha moja ya ndege iliyo kwenye uwanja wa ndege wa Olenya.
Kulingana na rekodi ya video, ndege nne ziliungua kwenye uwanja wa ndege - ikiwa ni Tu-95MS tatu na An-12 moja. Kulingana na wachambuzi wa OSINTtechnical, kulikuwa na Tu-95MS nne zilizoungua.
Picha mpya za satelaiti ambazo zingeonyesha wazi matokeo ya uvamizi huo bado hazijachapishwa.
Chanzo cha picha, https://www.youtube.com/@SecurityServiceUkraine
Operesheni 'Web'
SBU inadai kuwa operesheni hiyo, ambayo iliitwa "Mtandao", ilitayarishwa kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu, ikisimamiwa kibinafsi na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, na ilitekelezwa na mkuu wa Huduma ya Usalama ya Ukraine Vasyl Malyuk akishirikiana na wanajeshi wa huduma maalum.
Operesheni hiyo ilikamilika kupitia kkurushwa kwa ndege zisizo na rubani kutoka katika trela za malori ya mizigo ambayo yalikuwa yamekaribia kambi za wanaannga vituo vya anga.
"SBU kwanza ilituma ndege zisizo na rubani za FPV kwenda Urusi, na baadaye nyumba za mbao zinazohamishika," ripoti hiyo inasema. "Baadaye, kwenye eneo la Urusi, ndege hizo zisizo na rubani zilifichwa chini ya paa za nyumba ambazo tayari zilikuwa zimewekwa kwenye lori.
Wakati ulipowadia paa za nyumba hizo zilifunguliwa kwa mbali, na ndege zisizo na rubani ziliruka na kushambuliaji ndege za Urusi."
"Kwa mujibu wa sheria na desturi za kivita, tulifanya kazi kwa kufuata sheria za kivita kushambulia viwanja vya ndege za kijeshi na ndege ambazo hushambulia miji yetu ya amani," alisema Vasily Malyuk.
SBU ilisema kuwa zaidi ya theluthi moja ya ndege za kimkakati ziliharibiwa katika kambi za kijeshi za wanaanga wa Urusi.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla