Putin atalipiza kisasi kwa shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine, anaonya Trump

2 days ago 9

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wito wa Trump na Putin ulikuwa wa kwanza tangu shambulio kubwa la Ukraine dhidi ya ndege za kubeba makombora ndani kabisa ya Urusi

Vladimir Putin amesema atalazimika kujibu shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani za Ukraine dhidi ya vituo vya anga vya Urusi, Rais wa Marekani Donald Trump ameonya.

Akizungumza baada ya kupigiwa simu na rais wa Urusi, Trump alisema: "Rais Putin alisema, na kwa nguvu sana, kwamba atalazimika kujibu mashambulizi ya hivi majuzi kwenye viwanja vya ndege."

Maafisa wa Urusi walikataa kuthibitisha hili Jumatano usiku, lakini Moscow ilikuwa imesema hapo awali kuwa chaguzi za kijeshi "ziko mezani" kwa majibu yake.

Trump alionya katika chapisho la mtandao wa kijamii kwamba simu hiyo, iliyochukua zaidi ya saa moja, "haitaleta amani ya haraka" kati ya Urusi na Ukraine.

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Urusi- RIA Novosti, lilisema Putin alimwambia Trump kwamba Ukraine imejaribu "kuvuruga" mazungumzo na kwamba serikali ya Kyiv "kimsingi imegeuka kuwa shirika la kigaidi".

Mazungumzo kati ya viongozi hao wawili yanakuwa ya kwanza tangu Ukraine ilipofanya mashambulizi ya kushtukiza kwa kutumia ndege zisizo na rubani kushambulia vituo vya anga vya Urusi tarehe 1 Juni, yakilenga kile ilichosema kuwa ni washambuliaji wa masafa marefu wenye uwezo wa nyuklia.

Trump alimwambia Putin katika mazungumzo ya njia ya simu kwamba Marekani haikuonywa mapema kuhusu shambulio hilo, msaidizi wa rais wa Urusi Yury Ushakov alisema.

Wito wa Trump na Putin ulikuwa wa kwanza tangu shambulio kubwa la Ukraine dhidi ya ndege za kubeba makombora ndani kabisa ya Urusi

Read Entire Article