.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Utafiti umegundua kwamba 21% ya bahari ya dunia ni nyeusi

Dakika 8 zilizopita

Katika miongo miwili iliyopita, zaidi ya humusi ya bahari ya dunia imekuwa nyeusi, kulingana na utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Plymouth nchini Uingereza.

Utaratibu huu unajulikana kama " giza la bahari," na hutokea wakati mabadiliko yanapotokea kwenye sakafu ya juu ya bahari ambayo hufanya iwe vigumu kwa mwanga kupenya chini ya maji.

Eneo hili la juu la sakafu ya bahari huitwa "eneo la picha." Ni nyumbani kwa takriban 90% ya viumbe vya baharini na ni muhimu katika kudumisha mzunguko wa afya wa kimataifa wa biogeochemical.

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Global Change Biology, uligundua kuwa 21% ya bahari duniani zilifanya giza kati ya 2003 na 2022.

Utafiti unapendekeza kwamba bahari nyeusi inatokana na mchanganyiko wa mambo, ikiwa ni pamoja na maua ya mwani ambayo yamebadilisha mienendo yao, na mabadiliko ya joto la uso wa bahari.

Pia unaweza kusoma

Kwanini bahari inazidi kuwa nyeusi?

Mara nyingi tunaona rangi nyeusi zaidi katika maeneo ya pwani ambapo maji yenye virutubishi hupanda juu huku kuongezeka kwa mvua kukisafisha maji ya kilimo, kupeleka ndani ya bahari, na kusababisha kuongezeka kwa ukuaji wa plankton.

Mvua kubwa inazidi kunyesha katika sehemu nyingi za dunia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Katika bahari ya wazi, rangi nyeusi pia zimehusishwa na joto la juu la uso wa bahari, ambalo linaweza kusababisha kuongezeka kwa kuzuiwa kwa mwanga chini ya sakafu ya bahari.

Ni maeneo gani yalioathirika?

.

Chanzo cha picha, University of Plymouth

Maelezo ya picha, Mabadiliko katika maeneo ya kimataifa ya 'photic zones' kati ya 2003 na 2022. Nyekundu huashiria bahari nyeusi na bluu huashiria maeneo angavu zaidi.

Utafiti huo uligundua kuwa zaidi ya 9% ya bahari, eneo linalokaribia ukubwa wa Afrika, ilipata upungufu wa zaidi ya mita 50 za mwangaza, wakati 2.6% nyingine ya bahari ilipata upungufu wa zaidi ya mita 100 za mwangaza.

Utafiti huo pia uligundua kuwa mabadiliko makubwa zaidi katika kina cha eneo la picha 'Photic zone' yalionekana juu ya Ghuba Stream katika bahari ya Arctic na Antarctica, maeneo ambayo ulimwengu umeathiriwa zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa.

Rangi nyeusi pia ilienea katika bahari ya pwani na bara, ikiwa ni pamoja na Bahari ya Baltic.

Utafiti huu unasema kuwa giza la bahari sio tu kwa maeneo ya pwani, lakini pia huathiri bahari ya wazi.

Hatahivyo, utafiti uligundua kuwa sio sehemu zote za bahari ziliongeza giza, lakini karibu 10% ya bahari iling'aa kwa muda huo huo.

Waandishi wa utafiti wanasema mchanganyiko huu unaonyesha utata wa mfumo wa bahari na mambo mengi rangi ya maji.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Je, jambo hili linaathiri vipi viumbe vya baharini?

Ingawa athari halisi za mabadiliko haya bado hazijaeleweka, wanasayansi wanasema viumbe vingi vya baharini na mifumo ikolojia ya kimataifa inaweza kuathirika.

"Kuna utafiti unaoonyesha kuwa uso wa bahari umebadilika rangi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, labda kutokana na mabadiliko katika jamii za plankton," alisema Dkt. Thomas Davies, profesa msaidizi wa uhifadhi wa baharini.

"Lakini matokeo yetu yanatoa ushahidi kwamba mabadiliko kama haya yanasababisha giza kubwa zaidi, kupunguza eneo la bahari linalohitajika na wanyama wanaotegemea mwanga wa jua na mwezi ili kuishi na kuzaliana."

Tabaka hili la juu la maji ni makazi ya viumbe vingi vya baharini na ndiposa viumbe vinavyofanana na mimea vinavyoitwa phytoplankton hutafuta chakula. Viumbe hawa wadogo wako chini ya mnyororo wa chakula na wanaweza kupatikana karibu na uso kwa sababu wanahitaji mwanga wa jua ili kutoa chakula.

Ndiyo maana wanyama wengi wa baharini hula na kuzaliana katika 'photic zone', ambapo chakula ni kingi.

Phytoplankton pia huzalisha karibu nusu ya oksijeni katika angahewa na ni muhimu kwa ubadilishanaji wa gesi ya kaboni na maisha baharini.

"Sababu ya kweli ya wasiwasi"

Dkt. Davies anasema rangi nyeusi ya bahari inaweza kuwa na athari kwa hewa tunayovuta, samaki tunaokula na uwezo wa dunia wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

"Matokeo yetu yanaonyesha sababu halisi ya wasiwasi,"

Profesa Tim Smith, mkuu wa biogeokemia ya baharini na uchunguzi katika Maabara ya Plymouth, anasema baadhi ya wanyama wa baharini wanaweza kupanda juu ya uso wa bahari kutafuta mwanga, na tabia hii inaweza kusababisha kuongezeka kwa ushindani wa chakula na rasilimali nyingine.

"Hiyo inaweza kusababisha mabadiliko ya kimsingi katika mfumo mzima wa ikolojia wa baharini," Profesa Smith alisema.

Utafiti huu ulifanyikaje?

Katika utafiti huo kwa jina, "Rangi inayozidi kuwa nyeusi ya bahari Duniani{ The Deepening Color of the Global Ocean," watafiti walifanya uchambuzi wa miongo miwili wa data ya satelaiti.

Hifadhidata ya Rangi ya Bahari ya NASA inagawanya bahari za dunia katika pikseli za kilomita 9, hivyo kuruhusu watafiti kuchunguza mabadiliko katika uso wa bahari kwa kila pikseli, huku kanuni za algoriti zilizoundwa kupima mwangaza wa maji ya bahari zikitumiwa kukadiria kina cha eneo la picha katika kila eneo.

Miundo ya miale ya jua na mwezi pia ilitumiwa kuchunguza jinsi mabadiliko katika hali ya mwanga wa mchana na usiku yanaweza kuathiri wanyama wa baharini.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla