Usuhuba wa Trump na Musk unaonekana kumalizika rasmi baada ya kutupiana vitisho na matusi

1 day ago 8

g

Chanzo cha picha, Reuters

Usuhuba wa Rais wa Marekani Donald Trump na mfanyabiashara tajiri zaidi duniani Elon Musk sasa unaonekana kumalizika baada ya wawili hao kutupiana cheche za maneno makali na matusi kwenye mitandao ya kijamii.

Sasa Rais wa Marekani Donald Trump anasema "ameshangazwa sana" na "kukatishwa tamaa" na ukosoaji wa mshirika wa zamani Elon Musk kuhusu mswada wake mkuu wa bajeti .

"Mimi na Elon tulikuwa na uhusiano mzuri. Sijui ikiwa tutakuwa marafiki tena," Trump aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House siku ya Alhamisi.

Baada ya kauli hiyo, Musk alijibu kwa ujumbe mkali

Katika kujibu, Musk alimshutumu rais Trump kwa "kutokuwa na shukran", na kuongeza: "Bila mimi, Trump angepoteza uchaguzi".

Musk aliacha wadhifa wake katika Wizara ya Ufanisi wa Serikali wiki iliyopita baada ya siku 129 kazini, na Trump akamkabidhi ufunguo wa dhahabu wakati wa mkutano wa pongezi wa habari mnamo 30 Mei.

Lakini katika siku chache tangu aondoke mamlakani, Trump, amekuwa akiukosoa mara kwa mara a mswada wa bajeti ya Trump unaofanya kazi kupitia Bunge la Congress, akiuita wa " kuchukiza" na kuchapisha kwenye ukurasa wake wa X: "Aibu kwa wale walioipigia kura: unajua ulifanya vibaya."

Trump alichapisha kwenye mtandao wake wa Truth Social : "Njia rahisi zaidi ya kuokoa pesa katika Bajeti yetu, Mabilioni na Mabilioni ya Dola, ni kusitisha Ruzuku na Mikataba ya Kiserikali ya Elon. Siku zote nilishangaa kwamba Biden hakufanya hivyo!"

Kwa miaka mingi, Musk na makampuni yake wamepokea angalau $38 bilioni (£28bn) katika kandarasi za serikali, mikopo, ruzuku na mikopo ya kodi, kulingana na uchambuzi wa Washington Post.

Katika ujumbe mwingine wa Twitter, ambapo Musk alinakili chapisho la Trump, anasema: "Kwa kuzingatia kauli ya Rais kuhusu kufutwa kwa kandarasi za serikali yangu, @SpaceX itaanza kuzima chombo chake cha anga cha Dragon mara moja".

Dragon ndicho chombo ambacho kimekuwa kikiwapeleka wanaanga wa NASA angani.

Musk hakukomea hapo amezidisha ugomvi huu hata zaidi, akisema bila ushahidi katika chapisho jipya kwenye X kwamba Trump anaonekana kwenye faili ambazo hazijatolewa zilizoshikiliwa na serikali zinazohusiana na mfanyabiashara wa ngono- bilionea marehemu Jeffrey Epstein.

Mwaka jana, hati za mahakama zilizotolewa na jaji aliwataja watu wengi wa umma wanaohusishwa na Epstein. Trump alitajwa katika hati moja.

White House inasema madai ya Musk kuhusu Epstein ni 'bahati mbaya'

"Hiki ni kipindi cha bahati mbaya kwa Elon, ambaye hajafurahishwa na Mswada wa One Big Beautiful kwa sababu haujumuishi sera alizotaka," Katibu wa Habari wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt alisema.

Read Entire Article