Chanzo cha picha, Getty Images
Dakika 27 zilizopita
Liverpool wanatarajiwa kutoa ofa ya mwisho yenye thamani ya pauni milioni 118, kwa ajili ya kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz, 22, baada ya Bayer Leverkusen kukataa ofa ya awali ya pauni milioni 113 (Mail)
Everton wanavutiwa na kiungo wa Uingereza Jack Grealish, lakini uhamisho wowote unaweza kuwa wa mkopo kutokana na mshahara mkubwa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 pale Manchester City (Mail)
Real Madrid wanatarajiwa kufanya jaribio la mwisho kumsajili kiungo wa Real Sociedad mwenye umri wa miaka 26 kutoka Hispania Martin Zubimendi, ambaye yuko karibu kujiunga na Arsenal (AS - in Spanish)
Arsenal bado hawajafikia makubaliano na RB Leipzig kuhusu mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 22, lakini watafanya mazungumzo mengine wiki hii (Sky Germany)
Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 22, anasema hafikirii kuondoka Manchester United, licha ya kuhusishwa na uhamisho kwenda Inter Milan. (Talksport)
Kiungo wa Uingereza Myles Lewis-Skelly, 18, anatarajiwa kusaini mkataba mpya na Arsenal licha ya kuwepo kwa tetesi za kutakiwa na Real Madrid. (Football Insider)
Ofa ya Chelsea ya Euro milioni 35 (pauni milioni 29.5) kwa winga wa Uingereza Jamie Gittens imekataliwa na Borussia Dortmund, ambao wanataka Euro milioni 50-60 (pauni milioni 42-50) kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 (Sky Sports)
Chelsea wako tayari kuilipa AC Milan hadi Euro milioni 15 (pauni milioni 12.6) kwa ajili ya kipa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 Mike Maignan (Sky Sports)
Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa Verona na Italia Diego Coppola, 21, anasakwa na vilabu vya Bournemouth na Como msimu huu wa joto (Football Insider)
Mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen amekataa dili la Euro milioni 30 (pauni milioni 25.3) kwa msimu kutoka Al-Hilal, ambao walikuwa wamekubali kuilipa Napoli Euro milioni 75 (pauni milioni 63.2) kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ili kuvunja mkataba. (Football Italia)
Winga wa Uingereza na Manchester United Jadon Sancho, 25, ni mmoja wa wachezaji kadhaa ambao Al-Hilal wanataka kuwasajili msimu huu wa joto. (Foot Mercato - in French)
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Italia wanavutiwa na aliyekuwa meneja wa Chelsea, Leicester City na Roma Claudio Ranieri kumrithi Luciano Spalletti kama kocha mkuu wa Italia. (Football Italia)