JKT Queens yaanza na kocha

1 day ago 6

By  Nevumba Abubakar

Reporter

Mwananchi Communications Limited

WAKATI JKT Queens ikijiandaa na mashindano ya Cecafa ili kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika imeanza marekebisho ya benchi la ufundi ikidaiwa kumalizana na kocha mkuu Ester Chabruma ‘Lunyamila’.

Kocha huyo aliyehudumu kwa misimu miwili mfululizo tangu 2023 akichukua nafasi ya Ally Ally, ndiye aliyeipa ubingwa msimu huu na kulingana na Simba Queens kwa kutwaa mataji manne  ya Ligi Kuu ya Wanawake.

Chanzo cha kuaminika  ndani ya klabu hiyo, kimeliambia Mwanaspoti kuwa tayari JKT imempa Chabruma mkono wa kwaheri.

Mwanaspoti lilipomtafuta Ofisa Habari wa JKT, Masau Bwire alisema kama jambo hilo lipo basi litatangaza kwa vyombo vya habari. “Hizo ni tetesi tu kama jambo hilo lipo tutaita waandishi na kuweka kwenye mitandao yetu ya kijamii ila kwa sasa taarifa hizo sina,” alisema Bwire.

Kuondoka kwa Chabruma inaelezwa nafasi yake itachukuliwa na Mohamed Mrishona ‘Xavi’ aliyekuwa kocha wa timu ya vijana ya Simba. Chabruma alianza kibarua Julai 20, 2023 akianzia kwenye mashindano ya Cecafa baada ya JKT kubeba ubingwa wa ligi.

Alifanikiwa kubeba ubingwa huo mbele ya C.B.E ya Ethiopia akiitoa kwa penati 5-4 baada ya sare ya 1-1.

Ubingwa huo ulifanya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na kuishia hatua ya makundi. Chabruma ameipatia JKT Queens Kombe la Cecafa, Ngao ya jamii na Ligi Kuu yote yalikuwa Simba.

Read Entire Article