Nabi hajataka tamaa, atua tena Simba

1 day ago 4

By  Olipa Assa

Reporter

Mwananchi Communications Limited

Mambo ni moto! Siku chache baada ya nyota wa kimataifa wa Burkina Faso na Yanga, Stephanie Aziz KI kusajiliwa na Wydad Casablanca ya Morocco ni kama amefungua milango kwa mastaa wa Ligi Kuu Bara wanaowindwa na timu mbalimbali nje ya nchi.

Wakati Aziz KI akijiandaa kushuka uwanjani nchini Marekani kukipiga dhidi ya Manchester City, Juni 18, mwaka huu katika michuano ya Klabu ya Dunia ya Klabu, huku nyuma ameacha neema kwani kuna mstaa kibao wanahusishwa na timu mbalimbali zinazofuatilia kwa karibu maendeleo yao hapa nchini.

Na taarifa za karibuni ni kwamba kuna mazungumzo yanaendelea baina ya uongozi unaomsimamia mshambuliaji wa Simba, Steven Mukwala na Kaizer Chiefs kujadili dili la mchezaji huyo kama wanaweza kuununua mkataba wake uliobakia katika klabu hiyo hiyo ya Msimbazi.

Mukwala alisajiliwa na Simba msimu huu kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Asante Kotoko ya Ghana ambako alifunga mabao 14 na katika Ligi Kuu Bara anamiliki mabao 12 na asisti tatu.

Pendekezo la kuhitajika kwa Mukwala huko Kaiser Chiefs limetokana na kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ambaye alikuwa jukwaani wakati Simba ikishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Nabi anahusishwa pia na Jean Ahou na Joshua Mutale anaowataka kutoka katika kikosi cha Simba, huku pia akimtaka Feisal Salum 'Fei Toto' anayekipiga Azam FC.

Mwanaspoti limepata taarifa za ndani kwamba pamoja na Nabi kumtaka kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto' kinara wa asisti 13 ana mabao manane na Joshua Mutale pia ameona Mukwala ni aina ya washambuliaji wanaohitajika katika kikosi chake.

"Mukwala amebakiza mkataba wa miaka miwili, lakini kuna mazungumzo ya pande zote yanayoendelea itategemeana na ofa ya Kaizer Chiefs kama itakuwa na manufaa kwa mchezaji," kimesema chanzo hicho na kuongeza:

"Endapo Simba ikifanikiwa kumuuza Mukwala basi itambakiza Leonel Ateba aliye na mabao 12 ambaye yupo katika mstari wa kukatwa jina lake, pia kamati ya usajili tayari imeingia sokoni kumtafuta mshambuliaji wa kimataifa."

Mtazamo wa wadau
Akizungumza na Mwanaspoti, beki wa zamani wa Simba, Frank Kasanga 'Bwalya' amesema: "Simba inahitaji isajili wachezaji wenye uwezo wa juu wa kupambana katika michuano ya CAF, hilo litasaidia kuchukua ubingwa."

Mchezaji mwingine wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel amesema: "Simba ina kikosi kizuri lakini kinatakiwa kiongeze mshambuliaji mwenye maamuzi magumu na iendelee kuwajenga kiakili na uwezo waliyopo."

Read Entire Article