Chanzo cha picha, Getty Images
Dakika 32 zilizopita
Kiungo wa kati wa Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, anatarajiwa kufanyiwa vipimo huko Manchester City Jumapili ili kukamilisha uhamisho wake kutoka AC Milan. (Sky Sports)
Meneja wa Brentford Thomas Frank, ambaye anatazamiwa kuchukua nafasi ya Ange Postecoglou kama meneja wa Tottenham, anataka Spurs waingie kwenye mbio na Manchester United za kumsajili winga wa Bees kutoka Cameroon Bryan Mbeumo, 25. (Mirror)
Newcastle United wanatazamiwa kuongeza kasi ya kumsaka mshambuliaji wa Brighton na Brazil Joao Pedro, 23, baada ya kuonekana kumkosa Mbeumo. (Telegraph)
Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Ipswich Town Kieran McKenna yuko kwenye orodha ya Brentford ya wanaowezekana kumrithi Frank. (Sportsport)
Mlinzi wa kushoto wa Bournemouth Milos Kerkez ameachiliwa kutoka katika majukumu ya kimataifa na Hungary huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akikaribia kuhamia Liverpool. (Mirror)
Mlinzi wa Ureno Rafael Leao ameiambia AC Milan kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo, ambayo inataka angalau euro 70m (£59m) kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye ni mmoja wa walengwa wa Bayern Munich. (Florian Plettenberg)
Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wanatazamiwa kurejea na ofa ya pili kwa mlinda lango wa Ufaransa Mike Maignan, 29, baada ya kuwa na ofa ya kwanza, ambayo ni pungufu sana ya bei inayotakiwa na AC Milan, iliyokataliwa na timu hiyo ya Serie A. (Calciomercato)
Juventus wamefikia makubaliano na Paris St-Germain kuongeza muda wa mkopo wa mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, ili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 acheze na timu hiyo ya Serie A kwenye Kombe la Dunia la Vilabu la Fifa. (Sky Italy)
Mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 26, amekubali ofa ya kandarasi kutoka kwa klabu ya Saudi Pro League Al-Hilal. (Sky Italy)
Chanzo cha picha, Getty Images
Fenerbahce wameungana na klabu nyingine ya Uturuki Galatasaray kutaka kumsajili winga wa Ujerumani Leroy Sane, 29, ambaye bado hajakubali ofa ya mkataba mpya na Bayern Munich. (Sky Sports Ujerumani)
Bayern Munich wamefikia makubaliano na Bayer Leverkusen kumsaini mlinzi wa Ujerumani Jonathan Tah, 29, kabla ya mkataba wake kukamilika Juni 30 ili aweze kucheza Kombe la Dunia la Klabu ya Fifa. (Fabrizio Romano)