Chanzo cha picha, Getty Images
Dakika 13 zilizopita
Je, umehangaika kupata bidhaa zinazofaa kuitunza ngozi yako, na kuifanya ikufurahishe?...Ukweli ni kwamba bidhaa nzuri za utunzaji wa ngozi na utaratibu mzuri wa utunzaji wa ngozi ni muhimu ili kuwa na ngozi yenye furaha, yenye afya. Lakini kwa bidhaa zote zilizojaa madukani, utajuaje ni zipi zinazofaa kwako na mahitaji yako ya utunzaji wa ngozi?
Iwapo una matatizo kama vile kuwa na muwasho, chunusi, kukauka kwa ngozi au mabaka kwenye ngozi yako na umeshindwa kuyapatia suluhu? jibu la kwanza ni Fahamu mahitaji ya ngozi yako.
Kulingana na wataalamu mbali mbali wa ngozi, sio kila bidhaa unayoiona dukani au anayoitumia mtu mwingine unafaa kuitumia.
'' Watu wengi huwa na wazo kwamba mafuta au vipodozi yanayofaa kwa ngozi ya mtu fulani yatafaa pia kwa ngozi zao'', anasema Dkt . katika mazungumzo na Makala hii.
Kulingana na Daktari Catherine, matokeo ya mtu binafsi kwa bidhaa za utunzaji wa ngozi yanaweza kutofautiana kwani kila aina ya ngozi ina hitaji la kipekee''.
Chanzo cha picha, Getty Images
Mafuta au vipodozi vingi vya utunzaji wa ngozi huhudumia aina maalum za ngozi, kwahivyo ni muhimu kujua ngozi yako ni ya aina ipi kabla ya kuanza kufanya kuinunulia vipodozi vya utunzaji wake.
Jeni za urithi pia zina nafasi kubwa kubwa katika kuamua aina ya ngozi uliyonayo, sababu kama umri, hali ya hewa unyevu , mafadhaiko, na homoni ambazo zinaweza kuathiri pia.
Kuna auna au makundi matano 5 ya ngozi. Hizi zinatokana na kiasi gani cha sebum (dutu ya mafuta ambayo inalinda ngozi yako isikauke), au mafuta ya asili yanayozalishwa na ngozi yenyewe.
Mafuta : Inajulikana kwa uzalishaji wa kupita kiasi (tezi au vitu vyenye nta ambavyo hukausha mwili) wa sebum ( kiungo kinachohifadhi unyevunyevu wa mwili) ambayo husabaisha muonekano wa mg'ao wa ngozi, hupanua matundu ya mwili na huwa na tabia ya kusababisha kasoro kwenye ngozi.
Kavu : Unapokuwa na aina hii ngozi yako hupoteza maji na mafuta mengi, na mtu huishia kuwa kavu, mipasuko, na muwasho.
Mchanganyiko: kuna baadhi ya maeneo ya uso wako ambayo ni makavu na maeneo mengine ya uso wako ambayo yana mafuta zaidi. Kwa wale walio na ngozi ya mchanganyiko, eneo la T (paji la uso, pua, na kidevu) kwa kawaida huwa na mafuta, na mashavu mara nyingi huwa makavu zaidi.
Inayoweza kuathirika kwa urahisi (sensitive): Aina hii hufanya ngozi yako kukabiliwa zaidi na athari kama vile uwekundu, weusi na kuwasha. Watu wengi ambao wana ngozi hii hupata muwasho wa mara kwa mara , kuhusi kuungua , na huweza kupata mabaka ya ngozi.
Kawaida : Ngozi hii ni ngozi yenye uwiano mzuri inayofanana kila mahali, yenye muundo laini, vinyweleo visivyoonekana sana, ni laini na nyororo unapoigusa kwasababu ya uzalishaji
Bidhaa za ngozi zenye asidi ya juu ya oleic huwa na comedogenic zaidi, kumaanisha kuwa zina uwezekano mkubwa wa kuziba vinyweleo, hasa kwa watu walio na aina za ngozi za mafuta. Mafuta ya wastani na yasiyo na mafuta huruhusu ngozi kupumua lakini hulinda ngozi kutokana na unyevunyevu wa kupindukia.
Dkt: Catherine, Daktari wa magonjwa ya ngozi jijini Nairobi Kenya, anasema: ''Jambo kuu ni kujua aina ya ngozi yako iwe ni kavu, mafuta, nyeti, au mchanganyiko. Mara tu unapotambua hilo,chagua bidhaa zilizo na viambato laini na vyenye lishe kwa ngozi kavu kama vile keramidi, glycerini, na asidi ya hyaluronic, ambayo husaidia kudumisha kizuizi cha unyevu wa ngozi. Daima chagua chaguzi zisizo na harufu na hypoallergenic, ikiwa una ngozi nyeti na kwa ngozi ya mafuta chagua moisturizers nyepesi'',
Unaweza pia kusoma:'Tazama maelezo ya bidhaa ya kutunza ngozi/kipodozi'
Chanzo cha picha, Getty Images
Ni vyema kusoma maelezo ya bidhaa ya kipodozi au bidhaa za kutunza ngozi kabla ya kununua bidhaa dukani. ''Zingatia viambato muhimu vilivyounda bidhaa unayoinunua kubaini iwapo vinaendana na ngozi yako'', anashauri Daktari.
Kuna aina tofauti za bidhaa za ngozi kwa aina tofauti za ngozi na rangi. Aina tofauti za bidhaa za utunzaji wa ngozi zinalenga maswala mbalimbali, kila moja ikiwa na athari maalum kwenye ngozi. Bidhaa za kawaida ni pamoja na bidhaa za kusafisha (kwa kuondoa uchafu na mafuta), exfoliators (kwa kuondoa seli za ngozi zilizokufa), toners (kusawazisha pH ya ngozi), seramu (kwa matibabu yaliyolengwa), moisturizers (kwa ajili ya unyevu), mafuta ya macho (kwa eneo maridadi la macho), na mafuta ya jua (kwa ulinzi wa miale ya jua).
Baadhi ya bidhaa za utunzaji wa ngozi zina viungo ambavyo vinaweza kuwa na athari mbaya. Hizi ni pamoja na aina fulani za mafuta ya jua (kama vile zilizo na kiungo cha oxybenzone), exfoliants abrasive, bidhaa zilizo na vilevi (alcohol) nyingi au vihifadhi, na zile zilizo na kemikali zinazoweza kudhuru kama vile parabens, phthalates, au sulfates.
Kwa ujumla kipodozi kinachofanya kazi kwa mtu huyu kinaweza kisifanye kazi kwa mtu mwingine .
'Tunza ngozi yako'
Chanzo cha picha, Getty Images
Binafsi unahitaji kuitunza ngozi yako, hata kama una ngozi ya kawaida, hupaswi kuacha kuitunza - Hakikisha , inakuwa ngozi ya afya yenye, unyevu na kufuata utaratibu wa msingi ya utunzaji wa ngozi.
Ni bidhaa gani za ngozi zinapaswa kuepukwa?
Kulingana na Dr. Catherine ''Ni bora kuepuka bidhaa zilizo na kingo cha alcohok kikali, manukato ya syntetisk, na viwango vya juu vya mafuta'' . Anasema : ''Viungo hivi vinaweza kuharibu kizuizi cha ngozi na kusababisha muwasha, ukavu, au athari za mzio, haswa kwa watu walio na ngozi yenye hali fulani kama vile inayokabiliwa na eczema''.
Rangi nyeusi za ngozi inayoweza kuathirika kwa urahisi (sensitive) inaweza kuathiriwa kwa kwa viambato vya juu kama vile asidi ya alpha hidroksidi na asidi ya beta hidroksidi kuliko ngozi ya ya kawaida (tazama maelezo ya kipodozi).
Watu walio na ngozi nyeusi wanaweza kutumia retinoids zenye nguvu nyingi lakini lazima waanze polepole ili kuepuka kuathiri ngozi zao.
Wanapokuwa na muwasho wanaweza kupata hyperpigmentation (kupata mabaka kwenye ngozi) kwa urahisi zaidi kuliko aina nyingine za ngozi.
Je unawezaje kuitunza ngozi yako?
Chanzo cha picha, Getty Images
Epuka tabia zozote zinazoathiri ngozi yako moja kwa moja
Mambo mengi tofauti huathiri jinsi ngozi yako inavyoonekana na kuhisi. Hii, kwa upande wake, inathiri bidhaa za utunzaji wa ngozi utakazohitaji kutumia. Kwa mfano, kuvuta sigara au kutumia muda mwingi kwenye jua kunamaanisha kuwa utataka bidhaa zinazolenga uzalishaji wa collagen na uharibifu wa jua.
Kuwa na utaratibu wa kimsingi wa utunzaji wa ngozi: safisha kwa upole, lainisha kila siku, na utumie mafuta ya jua kila asubuhi—mvua au jua. Ngozi yenye afya inaonyesha ustawi wa jumla kwa hivyo unyevu, usingizi wa kutosha, mazoezi na kudumisha lishe bora ni muhimu sana katika afya ya ngozi , anasema Dkt Catherine.
Osha uso wako walau mara mbili kwa siku.
Visafishaji husaidia kuondoa mafuta yoyote, uchafu, na kitu kingine chochote ambacho kimekusanywa kwenye uso wako. Madaktari wa ngozi wanapendekeza kufinya kisafishaji kidogo kwenye vidole vyako na kukikanda kidogo kwenye ngozi yako. Kisha, suuza suds yoyote iliyobaki na maji ya joto kidogo, na ufute ngozi yako kwa kitambaa laini hadi iwe kavu kabisa. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo mahususi ya ngozi:
Tumia mafuta ya kujikinga na jua 30 ya SPF kila siku ili kulinda ngozi yako.
Kupigwa na jua kila siku kunaweza kuharibu ngozi yako kwa muda, kwa hivyo ni muhimu kuendelea kulinda.
Sugua mafuta ya jua kwenye sehemu zozote zilizo wazi za ngozi yako kama dakika 15 kabla ya kupanga kutoka nje.
Kumbuka kutumia bidhaa zisizo sahihi za utunzaji wa ngozi kunaweza kuathiri vibaya ngozi yako, na kusababisha athari kama vile kuwashwa, na kuzorota hali zilizopo kama vile chunusi, ukavu, au kubanduka kwa ngozi. Ni muhimu kuelewa aina ya ngozi yako na kuchagua mafuta ya mwili au bidhaa zinazoendana na aina yako ya ngozi ili kushughulikia mahitaji yake maalum.