Kiungo Prisons ataja sherehe kuikabili Yanga

6 hours ago 3

By  Saddam Sadick

Reporter

Mwananchi Communications Limited

Kiungo wa Tanzania Prisons, Kelvin Sabato amesema mchezo dhidi ya Yanga unaopigwa kesho ni kama sikukuu kwao, akieleza kuwa mechi hiyo siyo ya kutumia nguvu nyingi, bali akili pekee.

Wakati Sabato akitoa kauli hiyo, kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema wako tayari kuchukua pointi tatu ambazo zitaendelea kuwaweka katika msitari wa kutetea ubingwa huku akiitaja Dabi ya Kariakoo.

Prisons inatarajia kuwa uwanjani kesho dhidi ya Yanga, mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku kila timu ikiwa katika hesabu zake kwenye Ligi Kuu.

Yanga ndio wanaongoza katika msimamo kwa pointi 73, wakiwaaacha pointi moja watano zao Simba baada ya mechi 27, huku Prisons wakiwa na pointi 30 katika nafasi ya 13 na michezo miwili kumaliza msimu huu.

Akizungumza leo Juni 16, Sabato amesema mchezo huo pamoja na ugumu wake, lakini kwao ni kama sherehe na sikukuu kutokana na maandalizi waliyofanya kwa ajili ya ushindi.

Amesema kukutana na Yanga ni sehemu ya kuonesha ukubwa wa timu yao na wachezaji kwa ujumla akibainisha kuwa mechi hiyo si ya kutumia nguvu nyingi zaidi ya akili na maarifa.

"Mechi ngumu zinakuwa aidha dhidi ya Coastal Union na wengine, lakini kwa Yanga ni kuonesha ukubwa wa mchezaji na timu kwa ujumla, sisi kesho ni siku kuu, kila mchezaji anaitaka hii mechi," ametamba mchezaji huyo mkongwe katika soka la ushindani.

"Kocha ameshafanya kazi yake na haiingii yeye uwanjani. Mara kadhaa mchezo mgumu ni vile ukutane na aidha Coastal Union, kesho tutawaonyesha tunachotaka na mtaona."

Read Entire Article