Kinda la Yanga aondoka na mawili Uganda

12 hours ago 3

By  Nevumba Abubakar

Reporter

Mwananchi Communications Limited

KINDA la Yanga U-20 ambaye anaichezea Wakiso Giants ya Uganda kwa mkopo, Isaack Mtengwa amesema kumaliza msimu salama bila majeraha ni jambo jema kwake, akitaja mambo aliyojifunza kwenye ligi hiyo.

Huu ni msimu wa kwanza kwa nyota huyo kucheza Ligi Kuu Uganda kwani hapo awali alizichezea timu za vijana za Simba na Yanga na baada ya kufanya vizuri akatolewa kwa mkopo ili kupata uzoefu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mtengwa alisema nidhamu na kujituma ndiyo silaha kubwa ya mafanikio ya mchezaji na hilo ameliona kwenye ligi hiyo ambayo ina mchanganyiko wa wachezaji kutoka mataifa tofauti.

"Ni msimu mzuri na nimejifunza vingi sana kwenda kucheza ligi ya nje ya nchi, Ushindani wa namba ulikuwa mkubwa kwa sababu kila mchezaji alikuwa anapambana kuonyesha uwezo wake ili aingie kwenye kikosi na kusonga mbele zaidi."

Mbali na hilo kila mchezaji anakuwa na malengo yake binafsi na hapa anaeleza "Lengo la kwanza limetimia kucheza na kupata nafasi natamani pia kuitwa timu ya taifa ili na mimi nilitumikie taifa langu kwa sasa ni hayo."

Chama la nyota huyo limeshuka daraja likimaliza nafasi ya 15 kati ya 16 zinazoshiriki Ligi Kuu na kwenye mechi 30 imeshinda tatu sare 11 na kupoteza 16.

Read Entire Article