Wanne Twiga Stars watolewa CECAFA

12 hours ago 2

By  Nevumba Abubakar

Reporter

Mwananchi Communications Limited

NYOTA wanne wa kikosi cha timu ya taifa ‘Twiga Stars’ hawatakuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza mashindano ya CECAFA Senior Women’s Championship yanayofanyika Uwanja wa Azam Complex kutokana na ratiba za timu zao.

Nyota hao muhimu ni Julietha Singano na Enekia Kasonga wanaokipiga FC Juarez, Noela Luhala wa Asa Tel Aviv na Aisha Masaka ambaye aliumia kwenye mechi za kirafiki.

Inaelezwa ukimuondoa Masaka wengine wameruhusiwa kujiunga na timu zao na asilimia kubwa ya wachezaji wanaocheza nje wako mapumziko ya kumaliza ligi.

Enekia na Singano wako tayari kwenye majukumu ya timu yao ambayo iko Pre Season ikijiandaa na msimu mpya wa ligi ya Mexico.

Kikosi cha sasa kilichoundwa na kocha mkuu, Bakari Shime magolikipa ni Naijat Abbas wa JKT Queens na Asha Mrisho wa Mashujaa.

Mabeki ni Lidya Kabambo, Anastazia Katunzi, Christer Bahera wa JKT, Asha Omary wa Yanga, Fatuma Issa na Violeth Nickolaus wa Simba, Maimuna Hamis (Zed FC) na Ester Maseke (Bunda Queens).

Viungo ni Janeth Pangamwene, Donisia Minja na Winifrida Gerald (JKT Queens), Hasnath Ubamba (FC Masar) na Diana Msewa (Trabzonspor) huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Aisha Mnunka (Simba), Stumai Abdallah na Jamila Mnunduka (JKT), Opah Clement na Clara Luvanga (Al Nassr).

Read Entire Article