Burundi yaanza na ushindi CECAFA, yaichapa Uganda

1 day ago 5

By  Nevumba Abubakar

Reporter

Mwananchi Communications Limited

TIMU ya taifa ya Burundi imeanza vyema kampeni za kutafuta ubingwa wa mashindano ya CECAFA Senior Women Championship 2025 kwa kuichapa Uganda bao 1-0.

Mashindano hayo yanayopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamanzi yameanza leo Juni 13 na kutarajiwa kufikia kikomo Juni 25.

Bao la Esperancia Habonemana dakika ya 75 lilifanya mchezo huo kwenda dakika 90 Burundi ikiongoza licha ya ubora pamoja na mashambulizi waliyoyafanya Uganda.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kocha wa Burundi, Niyungeko Alain Olivier alisema watakwenda kufanyia marekebisho baadhi ya maeneo hasa kwenye kutengeneza nafasi.

"Tumepata ushindi muhimu ambao unawapa wachezaji wangu motisha ya kupambana, tumecheza mechi ya kwanza na Uganda ni timu nzuri sana,"

"Uganda wamekuwa wakitufunga sana lakini wachezaji wangu walijikaza na kama Uganda ingekuwa makini tungefungwa hata mabao mawili."

Kocha wa Uganda, Sheryl Botes alisema anajivunia namna timu ilivyocheza licha ya kupoteza mechi.

"Tunahitaji maandalizi ya kutosha, tunahitaji kupress mipira kwa sababu mechi hii tulikuwa nafasi ya kushinda kutokana na nafasi nyingi tulizotengeneza,"

"Tunahitaji kushinda mechi zijazo, tutakwenda kwenye kiwanja cha mazoezi kurekebisha tuliyokosea,"

Mechi nyingine itakayopigwa saa 1:00 usiku ni kati ya Tanzania na Sudan Kusini uwanjani hapo.

Read Entire Article