Walker

Chanzo cha picha, Getty Images

Dakika 26 zilizopita

Beki wa Manchester City na timu ya taifa ya Uingereza Kyle Walker, 35, amekubali kujiunga na Everton kwa mkataba wa mwaka mmoja. (Sun)

Mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, 25, anapigiwa upatu kuelekea Manchester United badala ua Tottenham Hotspur, licha ya mkufunzi wake wa zamani Thomas Frank kujiunga na Tottenham. (Sky Sports News)

Newcastle imeanza mazungumzo na Brighton kuhusu usajili mshambuliaji wa Brazil Joao Pedro, 22, na pia inavutiwa na beki wa Sporting Lisbon na Ivory Coast Ousmane Diomande, 21. (Telegraph - usajili unahitajika).

Juventus imempa mshambuliaji wa Sporting Lisbon Viktor Gyokeres kandarasi ya £11m kwa mwaka huku katika juhudi za kujaribu kuzipiku klabu za Arsenal na Manchester United kumsajili kwa mkataba mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 27. (Mirro)

Tottenham inatarajiwa kuanza mazungumzo na Rennes kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa Arnaud Kalimuendo, 23. (L'Equipe - kwa Kifaransa).

Manchester United imefanya mazungumzo ya awali na klabu ya Eintracht Frankfurt kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike, 22, lakini haijawasilisha ombi rasmi. (Sky Sports)

 Viktor Gyokeres

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Juventus yampa mshambuliaji wa Sporting Lisbon Viktor Gyokeres kandarasi ya £11m kwa mwaka

Napoli inapania kumsajili winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 20, au kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Jack Grealish, 29, lakini mabingwa hao wa Italia wako tayari kutumia £45m pekee. (Sun)

Atletico Madrid inawalenga beki wa Aston Villa na Ufaransa Lucas Digne, 31, ikiwa haitafanikiwa kumsajili beki wa Scotland na Liverpool Andy Robertson, 31. (Times - usajili unahitajika)

Chelsea imeanza mazungumzo na Lyon kuhusu usajili wa winga wa Ubelgiji Malik Fofana, 20. Nottingham Forest pia imeonyesha nia ya kumsajili winga huyo. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Kipa wa Barcelona na Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 33, amekataa ofa ya kujiunga na mabingwa wa Uturuki Galatasaray. (Sport - kwa Kihispania)

Alejandro Garnacho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Napoli inapania kumsajili winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho

Klabu za Athletic Bilbao, Marseille, Arsenal, Aston Villa, Inter Milan, na Napoli zimeonyesha nia ya kumsajili beki wa Al Nassr na Uhispania Aymeric Laporte, 31, ambaye zamani alikuwa Manchester City. (AS - kwa Kihispania)

Liverpool imeungana na Manchester United, Chelsea na Newcastle katika mbio za kumsajili winga wa Southampton na England U21 Tyler Dibling, 19. (CaughtOffside)

Pia unaweza kusoma:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi