,

Chanzo cha picha, Getty Images

19 Aprili 2024

Imeboreshwa Dakika 27 zilizopita

Mzozo unaoendelea kati ya Israel na Iran umezua taharuki kubwa duniani, ynanonesha wazi undani na hatari ya mwa mvutano wa mrefu kati ya mataifa haya mawili yenye ushawishi mkubwa Mashariki ya Kati.

Milipuko mikubwa ilisikika kote Tehran siku ya Ijumaa Juni 13, 2025, huku Israel ikitangaza kuwa imelenga maeneo ya nyuklia na vituo vya kijeshi.

Kwa sasa mapigano kati ya Israel na Iran yanaonekana kuwa ya mataifa hayo mawili pekee. Katika Umoja wa Mataifa na kwingineko kumekuwa na wito mkubwa mataifa hayo kujizuia kuendeleza mashambulizi.

Katika taarifa hii tunatathmini silaha za nchi zote mbili. Iran ina vifaru zaidi, meli za kivita na wanajeshi. Lakini mabilioni ya dola zilizotumika zaidi katika ulinzi wa Israel, ikilinganishwa na Iran, zimeisaidia kuunda vifaa vya kisasa zaidi - vingi vinavyotolewa na Marekani.

,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uwezo wa makombora wa Iran ni sehemu muhimu ya uwezo wake wa kijeshi

Ni nani mwenye nguvu za kijeshi zaidi kuliko mwingine?

BBC imeangazia swali hili kwa kutumia vyanzo vilivyoorodheshwa hapa chini, ingawa kila nchi inaweza kuwa na uwezo mkubwa ambao haujulikani.

Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo ya Kimkakati (IISS) inalinganisha nguvu ya silaha ya wanajeshi wa mataifa yote mawili, kwa kutumia mbinu mbalimbali rasmi na chanzo huria kutoa makadirio bora zaidi inavyoweza.

Mashirika mengine, kama vile Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, pia hufanya tathmini, lakini usahihi unaweza kutofautiana kwa nchi ambazo mara nyingi hazitoi takwimu.

IISS inasema Israel inatumia zaidi katika bajeti yake ya ulinzi kuliko Iran, ikiipa nguvu kubwa katika mzozo wowote unaoweza kutokea.

IISS inasema bajeti ya ulinzi ya Iran ilikuwa karibu $7.4bn mwaka 2022 na 2023, wakati ya Israel ilikuwa zaidi ya mara mbili ya hiyo, karibu $19bn.

Matumizi ya ulinzi ya Israel ikilinganishwa na Pato la Taifa pia ni maradufu ya Iran.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, F-35 ni mojawapo ya ndege za kisasa zaidi duniani

Faida ya kiteknolojia

Takwimu za IISS zinaonyesha kuwa Israel ina ndege 340 za kijeshi zilizo tayari kwa mapigano, na hivyo kuifanya iwe rahisi kufanya mashambulizi ya anga.

Miongoni mwa ndege hizo ni ndege za F-15 zenye masafa marefu, F-35s - ndege za teknolojia ya hali ya juu zinazoweza kukwepa rada - na helikopta zenye kufanya mashambulizi kwa haraka.

IISS inakadiria kuwa Iran ina takriban ndege 320 zenye uwezo wa kivita. Ndege hizo ni za miaka ya 1960 na ni pamoja na F-4, F-5s na F-14s (ya mwisho ni ndege iliyopata umaarufu katika filamu ya Top Gun ya 1986).

Lakini Nicholas Marsh wa PRIO anasema haijulikani ni ndege ngapi za zamani zinaweza kupaa, kwa sababu kupata vipuri itakuwa vigumu sana.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndege aina ya F-14 Tomcat iliondolewa na Jeshi la Wanamaji la Marekani karibu miaka 20 iliyopita, lakini bado inahudumu nchini Iran.

Mifumo ya Iron Dome na Arrow

Msingi wa ulinzi wa Israel ni mifumo yake ya Iron Dome na Arrow.

Mhandisi wa makombora Uzi Rubin ndiye mwanzilishi wa Shirika la Ulinzi la Makombora la Israel katika Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo.

Sasa ni mtafiti mkuu katika Taasisi ya Mikakati na Usalama ya Jerusalem, aliiambia BBC jinsi alivyohisi "salama" alipoona mfumo wa Iron Dome na washirika wa kimataifa wakiharibu karibu makombora yote na ndege zisizo na rubani ambazo Iran ilifyatulia Israel siku ya Jumamosi.

"Nilijisikia kuridhika na mwenye furaha sana... Ni mfumo wa kipekee dhidi ya maeneo yaliyo lengwa. Ni ulinzi wa makombora ya masafa mafupi. Hakuna kitu sawa na hicho katika [mfumo] mwingine wowote."

.

Chanzo cha picha, Amir Cohen / Reuters

Maelezo ya picha, Mfumo wa ulinzi wa makombora wa Iron Dome wa Israel ulisaidia kuharibu zaidi ya makombora 300 na ndege zisizo na rubani zilizorushwa na Iran mwishoni mwa juma.

Je, Iran iko umbali gani kutoka Israel?

Israel ni zaidi ya kilomita 2,100 kutoka Iran. Makombora yake ndiyo njia kuu ambayo ingeshambulia nchi hiyo, mhariri wa Jicho la Ulinzi Tim Ripley aliambia BBC.

Mpango wa makombora wa Iran unachukuliwa kuwa mkubwa na wa aina nyingi zaidi katika Mashariki ya Kati.

Mnamo 2022, Jenerali Kenneth McKenzie wa Kamandi Kuu ya Marekani alisema Iran ilikuwa na "zaidi ya makombora 3,000" ya balestiki.

Kulingana na Mpango wa Ulinzi wa Makombora wa CSIS, Israel pia inasafirisha makombora kwa nchi kadhaa.

.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Iran ilirusha zaidi ya makombora 300 na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel Jumamosi tarehe 13 Aprili

Makombora na ndege zisizo na rubani za Iran

Iran imefanya kazi kubwa katika mifumo yake ya makombora na ndege zisizo na rubani tangu vita vyake na nchi jirani ya Iraq, kuanzia mwaka 1980 hadi 1988.

Imetengeneza makombora na droni za masafa mafupi na marefu, nyingi zikiwa zimerushiwa Israel hivi karibuni.

Wachambuzi wanaochunguza makombora yaliyolengwa Saudi Arabia na waasi wa Houthi wamehitimisha kuwa yalitengenezwa nchini Iran.

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jengo la ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria liliharibiwa katika shambulizi la anga la Aprili 1, na kuua wanajeshi wakuu wa Iran.

'Kuadhibu' kupitia shambulizi la masafa marefu

Tim Ripley wa Defence Eye anasema Israel haina uwezekano mkubwa wa kujitosa katika vita vya ardhini na Iran: "Faida kubwa ya Israel ni nguvu zake za anga na silaha zake zinazoongozwa. Hivyo ina uwezo wa kuanzisha mashambulizi ya angani dhidi ya maeneo yake muhimu nchini Iran."

Ripley anasema Israel ina uwezekano mkubwa wa kuua maafisa na kuharibu mitambo ya mafuta kutoka angani.

"'Kuadhibu' ndio kiini chake... Viongozi wa kijeshi na kisiasa wa Israel wanatumia neno hilo kila wakati. Ni sehemu ya falsafa yao, kwamba wanapaswa kuwapa uchungu kuwafanya wapinzani wao kufikiria mara mbili kuhusu upinzani wao dhidi ya Israel."

Hapo awali, wanajeshi na raia mashuhuri wa Iran wameuawa katika mashambulizi ya anga, ikiwa ni pamoja na katika uharibifu wa Aprili 1 wa jengo la ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, ambao ulisababisha mashambulizi ya Iran.

Israel haijadai kuhusika na hilo au mashambulizi kadhaa yanayolenga maafisa mashuhuri wa Iran.

Lakini pia haijakataa kuwajibika.

.

Chanzo cha picha, IRGC handout / Reuters

Maelezo ya picha, Boti za mwendo kasi za Jeshi la Walinzi wa Iran zikiwa katika mazoezi katika Kisiwa cha Abu Musa

Vikosi vya wanamaji

Jeshi la wanamaji la Iran lililozeeka lina meli zipatazo 220, huku za Israel zikiwa na karibu 60, kulingana na ripoti za IISS.

,

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, IISS inasema jeshi la wanamaji la Israel lina takriban meli 60.

Tishio la nyuklia

Israel inadhaniwa kuwa na silaha zake za nyuklia, lakini inashikilia sera rasmi ya utata wa makusudi.

Iran haifikiriwi kuwa na silaha za nyuklia na, licha ya shutuma hizo inakanusha kuwa inajaribu kutumia mpango wake wa nyuklia wa kiraia kuwa taifa lenye silaha za nyuklia.

Jiografia na idadi ya watu

Iran ni nchi kubwa zaidi kuliko Israel na idadi ya watu wake (karibu 89m) ni karibu mara kumi ya Israel (karibu 10m).

Pia ina wanajeshi wanaohudumu mara sita zaidi ya Israel.

Kuna wanajeshi 600,000 wanaokaimu nchini Iran, huku Israel ikiwa na 170,000, inasema IISS.

.

Chanzo cha picha, Reuters

Israel inawezaje kulipiza kisasi?

Dr Eric Rondsky, mtafiti wa Mashariki ya Kati aliyehusishwa na Chuo Kikuu cha Tel Aviv, anasema Israel ilikubali kuwajibika kwa kushindwa kutangaza hali ya tahadhari wakati Iran ilipoishambulia.

Wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran katika nchi jirani hushambulia mara kwa mara maslahi ya Israel na wanaweza kuwa walengwa.

Jeremy Binnie, Mtaalamu wa Ulinzi wa Mashariki ya Kati, anaamini kuwa Israel haitaweza kulipiza kisasi mara moja: "Uwezekano, wana njia mbalimbali kama wangetaka kulipiza kisasi, kama vile kulipua kwa mabomu maeneo huko Lebanon au Syria."

Binnie ana mashaka kwamba kutakuwa na vita.

"Jeshi halitapigana, jeshi la wanamaji halitapigana, wao (Iran na Israel) wako mbali sana na kila mmoja wao. Anasema Israel italazimika kukiuka anga za nchi huru kama Syria, Jordan na Iraq.

Marekani imeishutumu Iran kwa kuwapa waasi wa Houthi wa Yemen ndege zisizo na rubani

Vita vya Israel na Iran kupitia 'washirika wao' ni nini

Ingawa Israel na Iran hazijapigana vita rasmi hadi sasa, nchi zote mbili zimekuwa kwenye mzozo usio rasmi.

Watu mashuhuri wa Iran katika mataifa mengine wanauawa katika mashambulizi yanayolaumiwa Israel, ikiwemo Iran, huku Iran ikiilenga Israel kupitia washirika wake.

Kundi la wanamgambo na kisiasa la Hezbollah linapigana vita vikali vya Iran dhidi ya Israel kutoka Lebanon.

Iran haikatai kuunga mkono Hezbollah.

Uungaji mkono wake kwa Hamas huko Gaza ni sawa.

Hamas ilianzisha mashambulizi ya Oktoba 7 dhidi ya Israel, na imerusha makombora kutoka Ukanda wa Gaza hadi katika maeneo ya Israel kwa miongo kadhaa sasa.

Israel na mataifa ya Magharibi yanaamini kuwa Iran inatoa silaha, risasi na mafunzo kwa Hamas.

.

Chanzo cha picha, Houthi militants handout / EPA

Wapiganaji wa Houthi wamekuwa wakiendesha mashambulizi kwenye meli katika Bahari ya Shamu.

Imefasiriwa na Asha Juma