Chanzo cha picha, Getty Images
Dakika 20 zilizopita
Manchester United wanaangalia chaguo lililopo endapo dili la Bryan Mbuemo litashindikana, Arsenal bado wanamtaka Viktor Gyokeres, Mathys Tel yuko tayari kuhamia Spurs kwa mkataba wa kudumu.
Manchester United itaelekeza macho yake kwa mchezaji wa Bournemouth wa Ghana Antoine Semenyo, 25, au kiungo wa kati wa Crystal Palace wa Uingereza Eberechi Eze, 26, ikiwa watashindwa kumpata mshambuliaji wa Brentford wa Cameroon Bryan Mbuemo, 25. (ESPN).
Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wako tayari kurejea na ofa nyingine ya kumnunua mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 27, huku Atletico Madrid pia wakimtaka mchezaji huyo. Gyokeres tayari amekataa kuhamia Manchester United. (Record - in Portuguese)
Tottenham Hotspur wanatarajiwa kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich Mathys Tel, 20, kwa mkataba wa kudumu baada ya kuwa nao kwa mkopo, hatua hiyo itakamilika hivi karibuni. (Bild - in German)
AC Milan wamewasiliana na Valencia kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Javi Guerra, 22. (Calciomercato - in Italian)
Pia unaweza kusoma:Chanzo cha picha, Reuters
Inter Milan wako tayari kupokea ofa kwa ajili ya kiungo mshambuliaji Hakan Calhanoglu, 31, huku Galatasaray ikionyesha nia ya kutaka kumsajili. (Gazetta - in Italian)
Southampton wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Cologne wa Marekani Damion Downs, 20. (Sky Germany)
Kocha Keith Andrews anafuatiliwa kuchukua nafasi ya Thomas Frank kama kocha wa Brentford. (Talksport)
Chanzo cha picha, Getty Images
Bayer Leverkusen inamtaka mshambuliaji wa Uholanzi Justin Kluivert baada ya kumuuza kiungo wa kati wa Ujerumani Florian Wirtz, 22, kwa Liverpool na wamewasiliana na Bournemouth kuhusu kupatikana kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Mail)
Kiungo mshambuliaji wa Uhispania Fer Lopez, 21, amekubali kujiunga na Wolverhampton Wanderers kutoka Celta Vigo lakini vilabu bado viko katika mazungumzo ya kima chake, huku kukiwa na mkanganyiko kuhusu kipengele cha kuachiliwa kwa mchezaji huyo. (Diario AS - in Spanish)
Chanzo cha picha, Gambia Football Federation
West Ham wamefanya mazungumzo kuhusu kumnunua mshambuliaji wa Gambia Adama Bojang, 21, kutoka Reims ya Ufaransa na wanaweza kumpata mchezaji huyo kwa pauni milioni 11. (Mirror)
Bournemouth wamekubali dili la kumsajili mshambuliaji Adrien Truffert, 23, kutoka Rennes, ambalo litamruhusu beki wa kushoto wa Hungary Milos Kerkez, 21, kukamilisha uhamisho wake kwenda Liverpool. (ESPN)
Wolves wanakabiliwa na ushindani kumbakisha kocha wao Mreno Vitor Pereira, huku Benfica wakiangalia uwezekano wa kumpeleka Lisbon. (Sun)