g

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Mtazamo wa mkakati wa kijeshi wa Marekani barani Afrika unabadilika chini ya Trump

Saa 1 iliyopita

Huku Rais wa Marekani Donald Trump akiwa katika njia ya kupunguza gharama tangu aanze muhula wake wa pili, misaada kwa Afrika imepunguzwa na sasa matumizi ya ulinzi yako machoni pake - lakini je, mbinu hizi zinaweza kuwa na gharama zaidi kwa muda mrefu?

Maneno ambayo utawala wake unashinikiza kwa Ulaya ni kwamba gharama za ulinzi ni "kugawana mzigo". Hii ndiyo changamoto ambayo Washington sasa inaitoa kwa majeshi ya Kiafrika pia - na hayana rasilimali za kutosha kuikabili.

Zaidi ya hayo, huku wakiwa wamebeba gharama kubwa ya maisha na pesa, katika mapambano ya kuzuia kuenea kwa makundi yenye silaha ya jihadi kote Sahel, bonde la Ziwa Chad na Somalia katika miaka ya hivi karibuni, wanaweza kusamehewa kwa kuhisi kwamba tayari wamebeba mzigo mkubwa - na kwasababu tu ya bara lao bali jamii ya kimataifa pia.

Benin, ambayo imepoteza zaidi ya wanajeshi 80 katika mashambulizi ya jihadi tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ni mfano mmoja tu.

g

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Maelezo ya picha, Moja ya malengo mapya ya magaidi hao ni kupata ufikiaji wa pwani ya Afrika Magharibi"

"Kitovu cha ugaidi duniani" ndivyo Sahel ilivyoelezwa siku chache zilizopita na Jenerali Michael Langley, ambaye kama mkuu wa Kikosi cha Marekani cha Afrika (Africom) anasimamia uwepo wa jeshi la Marekani kusini mwa Sahara.

Katika muhtasari na mahojiano katika wiki chache zilizopita, ameelezea kwa uwazi tisho ambalo makundi ya jihad yataleta ikiwa harakati zao za kuelekea kusini kuelekea Ghuba ya Guinea zitafanikiwa.

"Moja ya malengo mapya ya magaidi hao ni kupata ufikiaji wa mwambao wa Afrika Magharibi. Iwapo watapata fursa ya kuingia katika ufuo huo, wanaweza kufadhili shughuli zao kupitia magendo, biashara haramu ya binadamu na biashara ya silaha. Hili sio tu linayaweka mataifa ya Afrika hatarini tu lakini pia linaongeza uwezekano wa tisho la kuufikia mwambao wa Marekani."

Jenerali Langley amekiri kwamba ongezeko la sasa la mashambulizi ya wanamgambo "linatia hofu sana".

Hata hivyo pia mara kwa mara amesisitiza ujumbe wa msingi: Marekani ina nia ya kurejesha operesheni zake za kijeshi kusini mwa jangwa la Sahara, na kuacha majeshi ya ndani kuchukua mzigo zaidi wa ulinzi.

Baadhi ya wafanyakazi 6,500 kwa sasa wametumwa barani Afrika na jeshi la Marekani na orodha ya mwaka wa 2019 iliyochapishwa na Africom ilizitaja kambi 13 za Marekani "zinazodumu" katika bara zima na vituo vingine 17 vya muda.

Lakini baadhi ya kambi hizi, ikiwa ni pamoja na kambi iliyojengwa kwa madhumuni ya ndege zisizo na rubani huko Agadez nchini Niger, tayari zimefungwa, hasa baada ya vikosi vya kijeshi kunyakua mamlaka huko Niger, Mali na Burkina Faso tangu 2020.

Na sasa inaonekana kana kwamba utendaji wa Marekani iliyokuwa na tamaa utapunguzwa tena sana.

Labda tutaona nguvu zaidi za anga zikitumwa kutoka pwani ili kufikia malengo ya wanamgambo - Jenerali Langley anasema kumekuwa na mashambulio 25 nchini Somalia mwaka huu, mara mbili ya jumla ya 2024 - lakini kuna uwepo mdogo zaidi wa kijeshi wa marekani katika ardhi ya Somalia.

"Baadhi ya mambo ambayo tulikuwa tukiyafanya, huenda tusiyafanye tena," hivi majuzi aliuambia mkutano katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, uliowaleta pamoja wakuu wa majeshi na maafisa wengine wakuu kutoka nchi 37.

"Lengo letu si kutumika kama suluhu ya kudumu, bali ni kufikia malengo ya usalama ya Marekani ambayo yanaingiliana na washirika wetu. Tunapaswa kuwa na uwezo wa kuyasaidia mataifa ya Afrika kujenga uwezo wa kujitegemea wanaohitaji ili kukabiliana na ugaidi kwa uhuru na uasi."

Kwa ukali wa lugha yake Jenerali Langley anaanamaanisha mabadiliko makubwa ya mtazamo na sera ambayo yametokana na mabadiliko ya Januari ya mamlaka katika Ikulu ya White House.

"Tumeweka vipaumbele vyetu sasa - kulinda nchi."

Jenerali huyo aliweka bayana kile kilicho muhimu kwa utawala mpya wa Trump II, katika chapisho la Pentagon wiki iliyopita- kupambana na magaidi - hususan ambao wanaweza kuishambulia Marekani.

Vipaumbele vingine ni kukabiliana na kuenea kwa ushawishi wa kijeshi wa China kote barani Afrika na kulinda uhuru wa usafiri wa baharini kupitia maeneo muhimu ya biashara kama vile Milangobahari ya Gibraltar na Mediterania, Mfereji wa Suez na Mlango wa Bab el-Mandab kwenye mwisho wa kusini wa Bahari ya Shamu.

Unaweza pia kusoma:

g

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Marekani inashiriki katika michezo ya kila mwaka ya vita inayojulikana kama Africa Lion - hapa wanajeshi wa Morocco walishiriki mwezi uliopita katika zoezi la kupata bandari.

Kwa namna fulani, mwelekeo wa mafunzo na ujengaji uwezo ambao Jenerali Langley sasa anaufafanua si tofauti sana na mtazamo wa tawala za awali za Marekani, za Republican na Democrat.

Anapongeza mpango wa ushirikiano wa Jimbo la walinzi wa kitaifa, ambapo majimbo ya Marekani yamekuwa yakisaidia kujenga uwezo wa vikosi vya usalama vya serikali kote barani Afrika na sehemu nyingine za dunia - kwa miongo mitatu iliyopita.

Ufaransa pia inafuata mbinu hii, kwa kufungwa kwa kambi nchini Chad na Senegal, huku zile za Ivory Coast na Gabon zimekabidhiwa kwa serikali zao, na timu ndogo tu za mafunzo za Ufaransa zimesalia nyuma kufanya kazi pamoja na wenzao wa Kiafrika.

Hata hivyo, katika mambo mengine, mkakati wa utawala wa Trump barani Afrika unaonyesha kudorora kwa mitazamo na wakosoaji wanaweza kuhoji kujiondoa kwa uangalifu kutoka kwa kushughulikia sababu zinazosababisha kukosekana kwa utulivu, migogoro na ugaidi, hususan katika eneo la Sahel, ambalo ni kati ya maeneo masikini zaidi kwenye sayari.

Kwani chini ya Rais Joe Biden Marekani ilitazama mbali zaidi ya eneo la kijeshi pekee katika juhudi zake za kukabiliana na ongezeko la makundi ya jihadi na vyanzo vingine vya ghasia. Na Jenerali Langley, kama mkuu wa kikosi cha Africom, alikuwa mtetezi mkuu wa fikra hii pana zaidi.

Ni mwaka jana tu, katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press, apolielezea kile alichokitaja kuwa ni jibu la "serikali nzima" kwa kuongezeka kwa migogoro, akisisitiza umuhimu wa utawala bora na hatua za kukabiliana na udhaifu wa mataifa ya Afrika na athari za kuenea kwa jangwa, na mabadiliko ya mazingira.

Kwa mtazamo huu alitambua wazi kwamba kuandikishwa kwa makundi yenye silaha na kuenea kwa ghasia kunachochewa sio tu na itikadi za kijihadi, lakini pia na mambo mengi ya kijamii na kiuchumi, ikiwa ni pamoja na matatizo ya yanayoathiri maisha ya kilimo na wafugaji.

Jenerali Langley mwenyewe haonekani kuachana na uchambuzi huu, hivi majuzi akibainisha jinsi taifa la Ivory Coast lilivyokabiliana na tisho la wapiganaji wa jihad katika maeneo ya mpaka wake wa kaskazini kwa kuongezea vikosi vya usalama na miradi ya maendeleo.

Pia aliweza alisifu mafanikio ya mbinu kama hiyo iliyotekelezwa pia na rais wa Niger, Mohamed Bazoum, kabla ya kuondolewa madarakani katika mapinduzi ya Julai 2023.

g

Chanzo cha picha, Africom

Maelezo ya picha, Wajumb katika mkutano wa 2023 nchini Ghana wa Kikosi Kazi cha Malaria cha Afrika, mpango ulioanzishwa na Africom kusaidia kuratibu mapambano dhidi ya ugonjwa huo unaoua.

Lakini bila shaka, siku hizi Africom lazima ifanye kazi ndani ya muktadha wa sera ya kigeni ya Marekani iliyoundwa upya kwa kiasi kikubwa chini ya Trump.

Kuna hata uvumi kwamba inaweza kupunguziwa hadhi na kuwa kampuni tanzu ya kamandi ya Marekani barani Ulaya na Jenerali Langley anasema kuwa serikali za Kiafrika zinapaswa kuiambia Washington maoni yao kuhusu wazo hili.

Tayari kitengo tofauti cha Afrika katika Baraza la Usalama la Kitaifa lililopungua sana katika Ikulu ya White House kinaripotiwa kuunganishwa sehemu ya Mashariki ya Kati-Kaskazini mwa Afrika.

Mkurugenzi wake, Jenerali Jami Shawley, mtaalamu wa Afrika aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo mwezi Machi pekee, sasa amepewa majukumula kimkakati la jumla zaidi.

Akihutubia Bunge la Congress wiki hii , Jenerali Langley alionya kuhusu matarajio ya Uchina na Urusi katika bara la Afrika: wepesi wa Beijing wa kufaidika na kutokuwepo kwa Marekani na uwezo wa Moscow kuchukua fursa za kijeshi zinazotokana na machafuko na ukosefu wa utulivu.

Kwa kuzingatia wasiwasi huu, wengine wanaweza kujiuliza kama jenerali huyo ana mashaka yake kwa busara kuhusu mkakati uliopungua wa Afrika.

Wakati huo huo, chini ya "haja ya ufanisi" inayoongozwa, hadi hivi karibuni, na bilionea wa teknolojia Elon Musk, mashirika makuu ya maendeleo ya kimataifa ya serikali ya Marekani, USAID na Millennium Challenge Corporation, yamefungwa kwa ufanisi.

Ushirikiano mpya wa kiuchumi wa Marekani na Afrika sasa ni wa biashara na uwekezaji wa sekta binafsi.

Lakini biashara kwa ujumla inahitaji kufanya kazi katika mazingira thabiti na salama - ambayo kanda dhaifu na zinazokabiliwa na vurugu barani Afrika haziwezi kutoa.

Na katika kuhitimisha mashirika ya maendeleo ya Marekani, utawala wa Trump umejitenga na kufadhili miradi ya vijijini na programu za kijamii ambazo zilitaka kushughulikia shinikizo la ardhi na maji na ukosefu wa fursa za kiuchumi, vichochezi muhimu vya migogoro - na uajiri wa vikundi vya jihadi vya vijana wa vijijini waliokata tamaa.

Kwa maeneo tete ambayo ni vyanzo vikuu vya ghasia za kijihadi mwitikio wa Marekani umepunguzwa kwa kijeshi tu, na sasa inatafuta kuhamisha hata mengi ya hayo kwenye mabega ya mataifa ya Kiafrika ambayo tayari yanajitahidi kujibu ipasavyo changamoto na majukumu mengi.

Unaweza pia kusoma:

imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi