Chanzo cha picha, Brian Waihenya
- Author, Na Brian Waihenya na Damaris Kamande
- Nafasi, BBC Future Voices
- Akiripoti kutoka Nairobi
Dakika 26 zilizopita
Katika ulimwengu ambapo wazo la kuwawezesha wenye ulemavu kufikia huduma mara nyingi ni mawazo ya baadaye, watu wachache wenye mawazo mbadala wanaunda upya simulizi-uvumbuzi mmoja kwa wakati mmoja.
Wabunifu hawa hawabuni zana au vifaa; bali wanabuni uhuru, utu, na fursa kwa mamilioni ya watu wenye ulemavu. Kuanzia misaada ya msingi ya matembezi hadi teknolojia za mawasiliano za kimapinduzi, kazi yao ni ushuhuda wa nguvu ya mfumo jumuishi na huruma ya binadamu.
Hawa ni wavumbuzi watano ambao uvumbuzi wao sio tu unaharakisha maisha ya wenye ulemavu lakini pia usawa zaidi kwa watu wenye uwezo wote:
Unaweza pia kusoma:Angela Wanjiku - Ujumuishaji katika mtindo
Chanzo cha picha, Hisi Studio
Angela Wanjiku, mjasiriamali na mbunifu wa mitindo wa Kenya, ndiye mwenye maono nyuma ya Hisi Studio, chapa ambayo inafafanua upya mitindo kwa walemavu wasioona.
Miundo yake inajumuisha vipengele vya Braille na vya kugusa, kuruhusu wavaaji "kuhisi" mifumo na ujumbe kwenye nguo zao. Kila kipande pia kina nukuu za kuinua, kuongeza ujasiri na kuwa na mtazamo chanya
Kinachotofautisha Hisi Studio ni mbinu yake inayojali mazingira—kutumia nyenzo zinazoweza kutumika tena ili kupunguza taka.
Kazi ya Angela ni mchanganyiko mzuri wa mtindo, uendelevu, na athari za kijamii, na kuthibitisha kuwa mitindo inaweza kujumuisha na kuwajibika kwa mazingira.
Daniel Gatura – Kuendesha usafiri unaoweza kufikiwa
Chanzo cha picha, Daniel Gatura
Daniel Gatura ni mwanzilishi mwenza kampuni ya Ace Mobility, huduma ya usafiri inayoweza kufikiwa yenye makao yake nchini Kenya iliyoundwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Kwa zaidi ya safari 6,000 zilizowezeshwa, Ace Mobility inajitahidi kuziba pengo kubwa katika usafiri kwa kutoa chaguzi za usafiri za kuaminika, zinazojumuisha na zenye heshima.
Zaidi ya kuwezesha safari za wenye ulemavu, Ace Mobility imewezesha harakati kuelekea uhuru zaidi na ujumuishaji wa kijamii, kusaidia watu wenye ulemavu kuabiri miji yao kwa ujasiri na urahisi.
DJ Wiwa - DJ zaidi ya Mipaka
Chanzo cha picha, Brian Waihenya
Winfred Wanjiku Muchiri, anayejulikana kama DJ Wiwa, ni DJ wa Kenya ambaye alizaliwa na ugonjwa wa kupooza kwa ubongo. Kutumia miguu yake kuendesha zana za DJ, sio tu anafafanua upya kile kinachowezekana katika tasnia ya muziki lakini pia anatetea ujumuishaji wa walemavu katika nafasi za ubunifu.
Safari yake ilianza mnamo 2016, ikichochewa na kutiwa moyo na mama yake. Baadaye alijiandikisha katika Taasisi ya Talanta jijini Nairobi, ambako aliboresha ufundi wake. Hadithi ya DJ Wiwa ni moja ya uthabiti, talanta, na kwenda kinyume na dhana potofu.
Christopher Patnoe & Google tream - Tech fo All
Chanzo cha picha, Damaris Kamande
Akiwa mkuu ukifiwaji na ubunifu wa walemavu- Accessibility and Disability Innovation katika kampuni ya Google EMEA EMEA, Christopher Patnoe anaongoza juhudi za kufanya teknolojia iwe jumuishi zaidi.
Akiwa na uzoefu wa karibu miaka 30 katika makampuni makubwa ya teknolojia kama Apple na Disney, sasa anaangazia masoko yanayoibuka, ambapo mapungufu ya ufikiwaji wa teknolojia mara nyingi huwa makubwa zaidi.
Mojawapo ya miradi ya sasa ya Google inajumuisha programu inayotafsiri lugha ya ishara, na kufanya mitandao ya kijamii ipatikane zaidi kwa walemavu wa kusikia.
Kwa ushirikiano na wenzake Pascal Bijleveld na Prof. Cathy Holloway, Patnoe anasisitiza nguvu ya mabadiliko ya simu mahiri—hasa kwa walemavu wa kuona—na hitaji la muundo jumuishi katika huduma za kidijitali kama vile M-Pesa.
Deborah Maboya – Utetezi wa Elimu Jumuishi
Chanzo cha picha, Damaris Kamande
Deborah Maboya ni Mkuu wa Uendeshaji na Programu huko Thailand na Kiongozi wa Mradi wa Pamoja, ambao unatetea elimu jumuisi kwa watoto wenye ulemavu. Akiwa na historia ya sheria na usimamizi wa mradi, Deborah ameendeleza mikakati inayokuza ujumuishaji wa kijamii na fursa sawa kwa miaka sita.
Anapenda sana haki za afya ya ngono na uzazi (SRHR) kwa wanawake wenye umri mdogo wenye ulemavu. Kupitia majukwaa ya kidijitali kama vile programu ya OKY, anajitahidi kutoa elimu inayoweza kufikiwa kwa urahisi ya SRHR, hasa katika maeneo ya mbali na shule, kuwawezesha wanawake wenye umri mdogo kuwa na maarifa ambayo yanaweza kubadilisha maisha yao ya baadaye.
Wavumbuzi hawa watano sio tu wanabadilisha maisha - wanabadilisha mifumo. Kazi yao inatukumbusha kuwa uvumbuzi wa kweli unajumuisha, na kwamba tunapovumbua kwa huruma, tunajenga ulimwengu ambao kila mtu anaweza kustawi.
Wavumbuzi hawa watano sio tu wanabadilisha maisha - wanabadilisha mifumo.
Kazi yao inatukumbusha kuwa uvumbuzi wa kweli unajumuisha, na kwamba tunapovumbua kwa huruma, tunajenga ulimwengu ambao kila mtu anaweza kustawi.
Unaweza pia kusoma:Imetafsiriwa na Dnah Gahamanyi na kuhaririwa na Ambia Hirsi