Donald Trump akiwa katika mkutano wat G7 huko Alberta

Chanzo cha picha, Getty Images

  • Author, Tom Bateman
  • Nafasi, State Department correspondent
  • Saa 1 iliyopita

Kauli za Rais Trump kuhusu mzozo wa Israel-Iran zimebadilika kutoka kuunga mkono mashambulizi ya Israel hadi kujitenga na mashambulizi hayo kabisa na hatimaye kurejea tena alipoanzia.

Kutoeleweka kwake kumeibua utata huku mapigano yenyewe yakiongezeka.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema mashambulizi hayo "yaliratibiwa kikamilifu" na Marekani.

Lakini je, Trump anakabiliwa na changamoto zipi na atajinasua vipi kwenye mtego huo?

Pia unaweza kusoma

1. Kukubaliana na shinikizo za Netanyahu

Wakati makombora ya Israel yalipolenga mji wa Tehran Alhamisi iliyopita, Trump aliwatishia viongozi wa Iran akisema "tarajieni mashambulizi makali zaidi" kutoka kwa washirika wa Israel walio na mabomu ya Marekani.

Tunajua lengo kuu la Trump. Msimamo wake ni kama wa Netanyahu, kwamba Iran haiwezi kuruhusiwa kuwa na bomu la nyuklia. Muhimu zaidi, amesema chaguo analopendelea zaidi (tofauti na Netanyahu) ni kupitia makubaliano kati ya Marekani na Iran (njia hii pia inaakisi lengo lake la kujinadi kama mpatanishi wa kiwango cha kimataifa).

Lakini ana uhakika jinsi atakavyofikia lengo hilo, wakati mwengine anatumia vitisho , na wakati mwingine anatumia diplomasia. Wiki iliyopita kiongozi huyo alidiriki kusema kwa wakati mmoja kwamba mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran yatasaidia kufikia makubaliano au huenda "yakayasambaratisha".

Kutotabirika kwake wakati mwingine huashiriwa na wafuasi wake kama mkakati - nadharia inayoitwa "mwendawazimu" ya uhusiano wa kigeni. Nadharia hii ni ile ambayo hapo awali ilitumika kuelezea mbinu za mazungumzo za Trump na kupendekeza kwamba kutokuwa na uhakika wa kimakusudi au kutotabirika juu ya kitakachofanyika kunawashinikiza wapinzani (au hata washirika wa Trump) kutekeleza wajibu. Mkakati huu ulihusishwa sana na baadhi ya mazoea ya Vita Baridi vya Rais Richard Nixon.

Baadhi ya washauri na wafuasi wa Trump wanaunga mkono upande wa "shinikizo la juu" la nadharia ya wazimu linapokuja suala la mtazamo wake kwa Iran. Wanafikiri vitisho vitatawala mwishowe kwa sababu, wanahoji, Iran haiko makini kuhusu mazungumzo (ingawa mwaka 2015 nchi hiyo ilitia saini mkataba wa nyuklia ulioongozwa na Obama ambao Trump alijiondoa baadaye).

Smoke billows from the Tehran skyline as the Islamic Republic of Iran Broadcasting (IRIB) building has been hit by Israeli attack

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Smoke rises from explosion at state broadcasting building in Tehran

Netanyahu ametumia shinikizo la mara kwa mara kwa Trump atumie njia ya kijeshi na sio njia ya kidiplomasia, na rais huyo wa Marekani - licha ya hamu yake ya mara kwa mara ya kutaka kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel - mwishowe anaweza kuona haja ya kujibu vitisho vyake vya kivita zaidi kwa uongozi wa Tehran.

Israeli pia inaweza kuisukuma zaidi nyuma ya pazia Marekani kama inavyoona, kumaliza kazi hiyo. Marekani ina mabomu makubwa ambayo Israel inaamini kuwa yanaweza kuharibu eneo la Iran la kurutubisha madini ya uranium huko Fordow.

Mapigano yanapoongezeka, ndivyo shinikizo kwa Trump kutoka kwa kambi ya wanachama wa Republican katika Congress ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitaka mabadiliko ya utawala nchini Iran.

Trump pia ataona hoja kwamba anaweza kuwalazimisha Wairani kufanya mazungumzo naye wakiwa dhaifu. Lakini ukweli unabakia kuwa Wairani tayari walikuwa kwenye meza mazungumzo katika duru ya sita na mjumbe wa Trump Steve Witkoff yaliokuwa yamepangwa nchini Oman siku ya Jumapili.

Mazungumzo hayo sasa yameahirishwa.

2. Kuchukua msimamo wa katikati

Kufikia sasa, Trump amesisitiza kuwa Marekani haihusiki na mashambulizi ya Israel.

Kuongezeka kwa vita kuna hatari kubwa kwa uongozi wa Trump. Meli za kivita za wanamaji wa Marekani na betri za makombora ya ardhini tayari zinasaidia katika ulinzi wa Israel dhidi ya kisasi cha Iran.

Baadhi ya washauri wa Trump katika Baraza la Usalama la Kitaifa wana uwezekano wa kuonya dhidi yankufanya chochote kinachoweza kuongeza makali ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran katika siku za hivi karibuni, hasa kutokana na baadhi ya makombora ya Iran kuvunja ulinzi wa Israel na Marekani hadi kusababisha kifo.

Netanyahu sasa anahoji kwamba kumlenga Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei kungemaliza, na sio kuzidisha, mzozo.

Lakini afisa mmoja wa Marekani ambaye jina lake halikutajwa alifahamisha kwa baadhi ya vyombo vya habari mwishoni mwa juma kwamba Trump aliweka wazi kuwa anapinga hatua hiyo.

A building which was directly hit in Petah Tikva following an Iranian ballistic missile barrage

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Makombora ya balistiki ya Iran yaligonga majengo ya Tel Aviv

3. Kusikiliza sauti za Maga na kurudi nyuma

Moja ya sababu kubwa za kisiasa zinazocheza akilini mwa Trump ni uungwaji mkono wake wa nyumbani.

Warepublican wengi katika Bunge la Congress bado wanaiunga mkono Israel, ikiwa ni pamoja na kuendelea kusambaza silaha za Marekani kwa nchi hiyo. Wengi wameunga mkono kwa sauti mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran.

Lakini kuna sauti kuu ndani ya vuguvugu la Trump la Make America Great Again (Maga) ambao sasa wanakataa kabisa uungwaji mkono huu wa jadi wa "ironclad" kwa Israeli.

Katika siku chache zilizopita wameuliza kwa nini Marekani inahatarisha kuingizwa kwenye vita vya Mashariki ya Kati kutokana na ahadi ya Trump ya sera ya mambo ya nje ya ''Marekani Kwanza".

Mwandishi wa habari anayemuunga mkono Trump Tucker Carlson aliandika ukosoaji mkali siku ya Ijumaa akisema madai ya utawala wa kutohusika si ya kweli, na kwamba Marekani inapaswa "kuiangusha Israeli".

Alipendekeza Bw Netanyahu "na serikali yake yenye njaa ya vita" walikuwa wakitenda kwa njia ambayo ingewavuta wanajeshi wa Marekani kupigana kwa niaba yake.

Carlson aliandika: "Kushiriki katika hilo kutakuwa kidole cha kati katika nyuso za mamilioni ya wapiga kura ambao walipiga kura zao kwa matumaini ya kuunda serikali ambayo hatimaye itaweka Marekani mbele."

Vile vile, mwakilishi shupavu mwaminifu wa Trump wa Marekani, Marjorie Taylor Greene alichapisha kwenye X kwamba: "Yeyote anayezembea ili Marekani ishiriki kikamilifu katika vita vya Israel/Iran haungi mkono MAGA".

Maelezo ya video,

Hii inawakilisha udhaifu mkubwa kwa Trump.

Inaongeza shinikizo kwake kuona umbali wa mashambulizi ya Marekani na Israel na kuna dalili, hadharani angalau, kwamba amejibu.

Mjadala wa Maga mwishoni mwa juma uliambatana na yeye kuchapisha kwenye mitandao ya kijamii kwamba aliungana na rais wa Urusi Putin kutoa wito wa kukomesha vita.

Kufikia Jumapili alisema Iran na Israel zinapaswa kufanya makubaliano, na kuongeza: "Marekani haikuwa na uhusiano wowote na shambulio dhidi ya Iran".

Iran tayari imetishia kushambulia vituo vya Marekani katika eneo hilo ikiwa, kama inavyotokea sasa, Washington itasaidia ulinzi wa Israel.

Hatari ya majeruhi wowote wa Marekani inaweza kuona hoja ya Maga ya kujitenga na hivyo kuongeza shinikizo kwa Trump kujiondoa na kumtaka Bw Netanyahu kukomesha vita hivyo.