Chanzo cha picha, Getty Images
Dakika 3 zilizopita
Real Madrid inatumai kumsajili beki wa Liverpool Ibrahima Konate, 26, kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao, mkataba wa Mfaransa huyo utakapokamilika. (Marca - kwa Kihispania)
Arsenal inataka sana kuwamsajili mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 27, na mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 22, Lakini ina uwezo wa kumsajili mshambuliaji mmoja tu msimu huu wa kiangazi. (Miror)
Hata hivyo, Arsenal inahisi gharama ya kumsajili Gyokeres iko juu mno hivyo huenda ikaamua kumsajili Sesko au mshambuliaji wa Aston Villa wa Uingereza Ollie Watkins, 29. (Record - kwa Kireno).
Mshambuliaji wa Manchester United Rasmus Hojlund, 22, ameibuka kama shabaha kuu ya klabu ya Serie A Inter Milan. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Timu hiyo ya Old Trafford imeamua kumbakisha mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 24. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
Manchester United ilifanya mawasiliano na wawakilishi wa mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike, 22, anayechezea Eintracht Frankfurt, wikendi hii. (Bild)
Klabu za EPL za Chelsea, Aston Villa na Tottenham zinaendelea kumfuatilia winga wa Manchester United Alejandro Garnacho, 20, baada ya Muargentina huyo kuambiwa yuko huru kuondoka. (Mail)
Chanzo cha picha, Getty Images