JKU Princess yaanza na ushindi Ligi ya Wanawake Zanzibar

5 hours ago 3

By  Zuleikha Fatawi

Reporter

Mwananchi Communications Limited

JKU Princess imeanza vizuri Ligi Kuu Soka Wanawake Zanzibar (ZWPL) msimu wa 2024-2025, baada ya jana jioni Juni 16, 2025 kuichapa Warriors Queens mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Mao B uliopo Mjini Unguja.

Ligi hiyo ina jumla ya timu nne zinazoshiriki msimu huu wa 2024-2025 ambazo ni JKU Princess, Warriors Queens, Dunga Queens na Sauti Sisters zote zikitokea kisiwani Unguja.

Akizungumzia mwanzo mzuri wa kikosi hicho, Kocha wa JKU Princess, Michael Mfaume amesema ni kawaida ya mechi ya kwanza ya ligi kuwa ngumu kutokana na kila timu kujiandaa kuanza vizuri lakini anashukuru wamepata ushindi.

"Unapokutana na mpinzani wako katika mechi ya kwanza ni kujipanga kumaliza mchezo mapema na hilo lilifanikiwa japokuwa kuna baadhi ya maeneo tulikuwa dhaifu," amesema Mfaume.

Mfaume amesema kumalizika kwa mchezo huo anakwenda uwanja wa mazoezi kufanyia maboresho maeneo yenye upungufu ili mechi inayofuata wafanye vizuri zaidi.

Kwa upande wa Kocha wa Warriors Queens, Neema Machano, amesema sababu mojawapo iliyochangia kupoteza mchezo huo ni upya wa wachezaji waliopo kwani bado hawana muunganiko baina yao.

Read Entire Article