Ngasa, Dodoma Jiji suala la muda

1 day ago 4

By  Victoria Melkiad

Mwananchi Communications Limited

DODOMA Jiji imeingia sokoni mapema, huku ikiwa iko kwenye hatua za mwisho kumalizana na winga wa Tanzania Prisons, Benno Ngasa.

Benno ambaye mkataba wake na Tanzania Prison unamalizika mwishoni mwa msimu huu, ameichezea timu hiyo kwa miaka miwili huku akiwa miongoni mwa wachezaji tegemeo.

Taarifa za ndani kutoka Dodoma Jiji ilizonazo Mwanaspoti zinabainisha klabu hiyo imeshafanya mazungumzo na winga huyo na hivi karibuni atafika kuonana na mabosi wake wapya ili kusaini mkataba.

"Tuko kwenye hatua za mwisho kumsajili winga huyo kwani kilichobaki ni yeye kufika na kusaini mkataba wa miaka miwili.

"Tuna mpango wa kuunda timu ya wachezaji wenye nguvu, lakini pia wawe vijana ili kusaidiana na mastaa waliopo kujenga kikosi imara zaidi msimu ujao.

"Mipango ya msimu ujao ni mikubwa ndio maana tunataka kutanua kikosi ili kiwe na mastaa wengi wenye uzoefu," kilisema chanzo hicho.

Dodoma Jiji inashika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa imecheza mechi 28, imeshinda tisa, sare saba na kupoteza 12 ikifikisha pointi 34.

Kwa upande wa Tanzania Prisons, imecheza mechi 28, imeshinda saba, imepoteza 14 na sare sita ikiwa na pointi 30 katika nafasi ya 13, inapambana kutoka kwenye mstari wa kucheza mechi za mtoano kuwania kubaki Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao.

Read Entire Article