.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Vladmir Putin

Dakika 33 zilizopita

Mlipuko wenye nguvu unatokea kwenye kambi ya jeshi la Urusi. Miili ya marubani wawili wa F-35 inapatikana Norfolk. Urusi yatuma kundi la wanamaji kwenye ufuo wa Uingereza. Waziri Mkuu wa Uingereza awaita kwa dharura mawaziri, wanajeshi na maafisa wa ujasusi kwenye mkutano.

Huo ndio mwanzo wa kipindi cha podikasti cha The Wargame, kinachojumuisha vipindi viwili vya kwanza ambavyo vilitolewa wiki hii na kituo cha televisheni cha Uingereza Sky News na tovuti ya habari Tortoise Media.

"Mwaka mmoja baadaye, uliorekodiwa kwa siku moja tu," anasema mwandishi mwenza wa podcast Deborah Haynes, mhariri wa kijeshi wa Sky News. "Katika Michezo ya Vita tunachunguza tishio ambalo Urusi ya Vladimir Putin inaleta kwa Uingereza, watu wake na maisha yao ya kila siku."

Kwa kuongezea, kulingana na Haynes, waandishi na washiriki wa WarGames wanagundua jeshi la Uingereza liko katika hali gani miaka 30 tangu kuanguka kwa Muungano wa Soviet.

Kwa kuongezea, waandishi wa podcast walifikiria jinsi washirika wa Uingereza, haswa Marekani ikiongozwa na Rais Donald Trump aliyejitenga, wangejibu vipi tishio la mzozo huo.

Maandishi ya mchezo huo yaliandikwa na Dkt. Rob Johnson, mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Oxford, Kituo cha Mabadiliko ya Hali ya Vita, na kuwaweka nyota baadhi ya wanasiasa na wataalamu mashuhuri wa Uingereza.

Wadhfa wa Waziri Mkuu wa Uingereza unaigizwa na Waziri wa Ulinzi wa zamani katika serikali kadhaa za kihafidhina Ben Wallace (alishikilia wadhifa huu mwanzoni mwa vita kamili vya Ukraine na akauacha mnamo Septemba 2023).

Waziri wa Mambo ya Nje ni mwanasiasa mkongwe wa Uingereza na Mbunge wa Leba Jack Straw, ambaye kwa nyakati tofauti aliongoza wizara mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Mambo ya Nje.

Wadhfa wa Katibu wa Mambo ya Ndani pia utaigizwa na Katibu wa zamani wa Mambo ya Ndani Amber Rudd.

Viongozi wa kijeshi wa Uingereza katika podikasti hiyo wataigizwa na majenerali waliostaafu.

"Kremlin Briefing" ya podcast inaongozwa na mtaalamu wa Urusi Keir Giles, mwandishi wa vitabu kadhaa vikiwemo Vita vya Urusi dhidi ya Kila Mtu .

Anafafanua kuwa katika aina hizi za michezo ya vita, "timu nyekundu", inayocheza adui anayewezekana, ina mpango na inajua mapema kile inakusudia kufanya.

Timu inayocheza na serikali ya Uingereza inalazimika kufanya kazi kusikojulikana.

Majibu ya Moscow kuhusu podcast hii mpya hayajulikani. Maafisa wa Urusi wamekanusha mara kwa mara nia yoyote ya kushambulia nchi za NATO; Rais Vladimir Putin, kwa mfano, alijibu swali la moja kwa moja kuhusu hili mwaka mmoja uliopita kwa maneno yafuatayo: "Je!

Katika mahojiano na BBC mwezi Aprili, balozi wa Urusi mjini London, Andrei Kelin, pia alikanusha kuwa Urusi ilikuwa tishio kwa Uingereza.

Kremlin inaonyesha uvamizi wake wa Ukraine kama hatua ya lazima na inalaumu Magharibi kwa kuanzisha vita.

Pia unaweza kusoma

.

Chanzo cha picha, SKY NEWS

Maelezo ya picha, Wanachama wa serikali na viongozi wa kijeshi kwenye podikasti wanaigizwa na wanasiasa na viongozi wa kijeshi wa kweli na maarufu sana.

Ili kurekodi podikasti, Kobe alikuwa na "mahandaki" matatu yaliyowekwa kwenye eneo la chini la nyumba yao, kama yale ya kweli pamoja na meza za mikutano na vichunguzi na ramani ukutani.

Vipindi vya kwanza vya saa mbili vya podcast vilitolewa mnamo Juni 9, vingine viwili vitatolewa tarehe 17, na sehemu ya mwisho, ya tano, itatolewa mnamo Juni 24.

Miaka tisa iliyopita, miaka miwili na nusu baada ya Urusi kuteka Crimea na kuanzisha vita vya ndani huko Donbas, BBC ilifanya kitu sawa na Michezo ya Vita.

Kampuni ya televisheni ilitoa filamu iitwayo WW3: Inside the War Room, ambayo ilicheza kisa cha kudhahania cha vita vya nyuklia na Urusi.

Maundui ya mchezo huu yanaanza na waasi wanaoiunga mkono Urusi, kwa msaada wa Urusi, wakiteka jiji la Daugavpils, jiji la kusini mashariki mwa Latvia, karibu na mpaka na Belarusi, ambapo idadi kubwa ya watu wanazungumza Kirusi.

Kisha wanachukua udhibiti wa miji mingine ya mashariki mwa Latvia, pamoja na sehemu ya mpaka na Urusi, na kutangaza "jamhuri ya watu" (kama ilivyotokea mashariki mwa Ukraine mnamo 2014) - na hali hiyo inakua hadi "baraza la mawaziri la vita" la Uingereza linapaswa kuamua kuhusu kuanzisha shambulizi la nyuklia kwenye malengo nchini Urusi katika ulinzi wa mshirika wa NATO Latvia.

Urusi tayari imeshutumu waundaji wa filamu hiyo kwa kufanya uchochezi

Balozi wa Urusi wa wakati huo huko Latvia, Alexander Veshnyakov, alisema kwamba waundaji wa filamu hiyo walikuwa wakiichafua Urusi na kujaribu kudharau nguvu za kisiasa za Latvia na Uropa .

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla