Marekani kuondoa sehemu ya ubalozi wake nchini Iraq huku mvutano na Iran ukiongezeka

1 day ago 2

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Marekani inajiandaa kuwaondoa wafanyakazi wake na familia zao kutoka ubalozi wake nchini Iraq pamoja na wale walio katika kambi za kijeshi nchini Kuwait na Bahrain.

Maafisa wanasema hatua hiyo ni kufuatia hatari za kiusalama zinazojitokeza katika kanda hiyo.

Maafisa hawakusema ni nini hasa kilisababisha kuondolewa, hata hivyo, siku ya Jumatano, maafisa wa Marekani waliambiwa kuwa Israel ilikuwa tayari kuanzisha operesheni nchini Iran, iliripoti mshirika wa BBC wa Marekani CBS, akinukuu maafisa wanaofahamu suala hilo.

Maafisa hao walisema hii ni sehemu ya sababu ya Marekani kuwashauri baadhi ya Wamarekani kuondoka katika eneo hilo, na kwamba Marekani ilitarajia Iran ingeweza kulipiza kisasi katika baadhi ya maeneo ya Marekani nchini Iraq.

Mjumbe wa Marekani katika Mashariki ya Kati Steve Witkoff bado anapanga kukutana na maafisa wa Iran kwa awamu ya sita ya mazungumzo siku ya Jumapili, maafisa hao waliiambia CBS.

Afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani aliiambia BBC: "Tunatathmini mara kwa mara usalama wa wafanyikazi katika balozi zetu zote.

"Kulingana na utafiti wetu wa hivi punde, tumeamua kupunguza uwepo wetu katika misheni yetu nchini Iraq."

Trump alizungumza kuhusu Iran katika mwonekano katika Kituo cha Kennedy siku ya Jumatano, akiwaambia waandishi wa habari Wamarekani walishauriwa kuondoka katika eneo hilo "kwa sababu inaweza kuwa mahali pa hatari, na tutaona kitakachotokea."

Trump pia alisisitiza kwamba Marekani haikutaka Iran kutengeneza silaha ya nyuklia: "Hatutaruhusu hiyo."

Rais ana matumaini ya kufikia makubaliano ya kuzuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia.

Awali, Rais wa Marekani Donald Trump alisema anapoteza imani kuhusu mazungumzo yanayoendelea kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran na amekuwa akitishia kuishambulia Iran iwapo mazungumzo yatafeli huku Iran ikiapa kuzilenga kambi za kijeshi za Marekani zilizoko kanda ya Mashariki ya Kati iwapo itashambuliwa.

Soma zaidi:

Read Entire Article