Foto

  • Author, Tamara Ebiwei
  • Nafasi, BBC News Pidgin
  • Dakika 16 zilizopita

"Wafugaji walivamia eneo hilo, kwanza walitukamata baadhi yetu [wanawake] na kutuweka sehemu tofauti kabla hawajaanza kushambulia na kuwapiga risasi na kuwaua wanaume ambao hawakuwa na bahati ya kunusurika."

Ndivyo alivyosimulia manusura mmoja kutoka jamii hiyo, Edikwu Ankpali, kutoka eneo la Apa, jimbo la Benue, Nigeria ambapo watu wanaodhaniwa ni wafugaji wanashukiwa kufanya unyama huo.

Watu hao wanaoshukiwa walishambulia jamii hiyo kati ya Jumapili Juni Mosi na Jumatatu Juni 2. Watu kadhaa waliuawa, na sasa, tunasikia hadithi kutoka kwa wanawake ambao wanaeleza walibakwa. Zaidi ya wanawake kumi katika jamii hiyo waliripotiwa kubakwa, baadhi yao bado wako hospitalini.

Wanawake wanasimulia maumivu ya kihisia na kimwili waliyokumbana nayo mikononi mwa washambuliaji. Mmoja wa waathirika aliiambia BBC Pidgin kwamba walimbaka mara nane ndani ya saa saba. Alisema baada ya kuanza kuwashambulia baadhi ya wanaume, walianza kuwabaka wanawake kwa makundi katika jamii hiyo.

"Walinibaka mara nane kabla ya alfajiri, wengine mara 10. Wafugaji hao walikuwa kama 50 hivi," alisema.

Kiongozi wa vijana Odogbo Ngbede pia aliiambia BBC Pidgin kwamba, "hatujui wake zetu walipo tena," hii ikiwa ni kutokana na baadhi ya wanawake bado hawajulikani walipo.

Mhanga mwingine alisema alikuwa amekaa na baba yake ambaye ni mzee na mgonjwa kabla hawajaja. "Walimuua baba yangu, kisha wakanibeba na kunipeleka sehemu kunibaka," alisema mwanamke huyo kwa huzuni.

Wanawake hao waliiambia BBC Pidgin kwamba wana maumivu kwani wameshindwa kutembea vizuri kwa siku kadhaa sasa. Waathirika wa ubakaji inaelezwa walikuwa na umri wa kati ya miaka 35 na 60.

"Nimepoteza ndugu sita wa familia yangu"

Bibi Sarah (sio jina lake halisi) aliyekimbia kijijini kwenda makao makuu ya serikali za mitaa aliiambia BBC Pidgin kwamba, wafugaji wanaoshukiwa wamemfukuza kutoka kijijini kama wengine pia wanaokimbia.

Alisimulia kuwa walimuua baba yake aliyekua mzee na baadhi ya binamu zake na hadi sasa, hawajaona miili yao. Aliongeza kuwa kama wangekuwa hai, wangekuwa na wenyewe wangekuwa wamekimbia kujificha kwa usalama.

"Waliuua karibu familia yangu yote, sitarudi tena isipokuwa kama serikali itafanya jambo kutusaidia. Kama amani haitarudi kijijini kwangu, sitarudi."

"Njaa inatuua, hatuwezi tena kwenda kulima, nimelala nje muda wote huu, kabla sijakimbia kutoka kijijini walikuwa wameua watu 29." Alisema ni kwa neema ya Mungu alinusurika.

One of di victims of di suspected herders attack, na man wey lie down for bed wey no wear cloth to show im injury.

Maelezo ya picha, Foto of one of di victims wey wound

"Tunakabiliwa na mazito' - Gavana Alia

Gavana wa Jimbo la Benue Hycinth Alia alizungumza kwenye mahojiano na Channels TV akisema haoni tena mashambulizi hayo kama mapigano kati ya wakulima na wafugaji.

Alisema watu wenye uhusiano na magaidi wanafanya hivyo kama vile wanapigana vita vya msituni. "Jinsi mashambulizi haya yanavyokuja na taarifa tunazopokea, ni mpango wa moja kwa moja na uliopangwa na watautekeleza. Kila siku, tunapokea taarifa hizi. Hivi karibuni, kila taarifa tunayopokea, asilimia 60 hadi 65 yake ni sahihi kabisa."

"Na kisha ukigundua kinachoendelea, kimezidi kuwa mgogoro tu, kimezidi kuwa mapigano ya kikabila kati ya wafugaji na wakulima katika jimbo letu, yameelekezwa, yamepangwa na kisha, watayatekeleza, huu ni ugaidi."

"Kwa sababu fulani, hawawezi kuwakamata hata mmoja wao. Wanakuja usiku wa manane, wanashambulia na kukimbia na hakuna anayeona dalili zozote. Hivyo, ni ugaidi unaotumaliza," alisema.

Watu wanaodahniwa ni wafugaji walivamia na kushambulia wakazi wa Tse-Antswam katika mji wa Naka, na Edikwu Ankpali katika eneo la serikali za mitaa la Apa, jimbo la Benue kati ya Jumapili Juni 1 na Jumatatu Juni 2.

Zaidi ya watu 50 walikufa katika shambulio hilo na baadhi ya watu bado hawajulikani waliko.