Kumekuchaa! Kisa Dabi viongozi Yanga waitwa TPLB

13 hours ago 3

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Communications Limited

WAKATI sintofahamu ikiendelea kutanda juu ya hatma ya mchezo wa Dabi ya Kariakoo, viongozi wa juu wa Yanga wameitwa makao makuu ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB).

Taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inaeleza TPLB imewaita viongozi hao mezani, kuzungumza nao kwani Yanga ndiyo timu mwenyeji wa mchezo huo.

Kwenye kikao hicho, bodi ya ligi inawataka viongozi hao wa Yanga kueleza hatua ya maandalizi ya mchezo huo ambao umepangwa kupigwa Juni 15, 2025.

Hatua hiyo inakuja zikiwa zimesalia siku saba kuanzia siku ya kikao hicho na kitafanyika makao makuu ya bodi hiyo, yaliyopo Ilala, jijini Dar es Salaam.

"Kutakuwa na kikao cha bodi na timu mwenyeji kitakachofanyika Jumatatu Juni 9, 2025 na kuanzia hapo tutajua nini kitaendelea. Hiki ni kikao cha kawaida tu cha maandalizi ya mchezo," amesema bosi huyo wa juu ndani ya TFF.

Kikao hicho kitafanyika wakati Yanga bado ikiwa kwenye msimamo mkali wa kutokucheza mchezo huo, kwa madai chombo hicho hakijayafanyia kazi masuala yaliyosababisha kuahirishwa kwa ule wa kwanza uliopangwa kufanyika Machi 8, 2025.

Hata hivyo, Yanga inaona kikao hicho ni kam mtego, kwani hakujawahi kufanyika mkutano wa namna hiyo utakaowakutanisha uongozi mzima wa juu wa Yanga.

Kwenye kikao hicho Yana imetakiwa kuwakilishwa na kamati nzima ya utendaji kuanzia Rais wa klabu hiyo Injinia Hersi Said, Makamu wake, Arafat Haji na wajumbe wa kamati yao ya utendaji.

Mchezo huo ambao haijajulikana utapigwa kwenye uwanja upi, bado umeacha maswali iwapo utakuwepo au la, huku badhi ya nyota wa vikosi vyote walioitwa timu ya Taifa, Taifa Stars wakirejea

kutoka Afrika Kusini kujiunga na wenzao baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Wasauzi uliomalizika kwa suluhu na ulipigwa nchini humo, ijumaa usiku.

Kikosi cha Yanga kimekuwa kikiendelea na mazoezi na inaelezwa ni kujiandaa na michezo mitatu iliyosaliwa nayo, miwili ya Ligi Kuu Bara, dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji, pamoja na ule wa fainali ya Kombe la FA, dhidi ya Singida Black Stars.

Read Entire Article