Zoezi la kuwaandikisha wapiga limezinduliwa jijini Mogadishu, Somalia

Somalia imezindua zoezi la kuwaandikisha wapiga kura, jijini Mogadishu, kwa mara ya kwanza baada ya miaka hamsini, ikiwa ni jitihada za kuwaanda wananchi wa taifa hilo kushiriki kwenye zoezi la kuwachagua viongozi wao kwa kura mwaka ujao.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja, baada ya rais Hassan Sheikh Mohamud, mwaka uliopita, kuahidi kumaliza zoezi la uchaguzi kwa mfumo wa koo, ambao umekuwa ukitumiwa  tangu mwaka 1969.

Kundi dogo la wakaazi wa Mogadishu, wameonekana wakiwe kwenye foleni kujiandikisha, wakati huu pia taifa hilo la pembe ya Afrika linapojiandaa kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali ya mitaa mwezi Juni.

Wakati wa uchaguzi huo, raia wa Somalia, wanatarajiwa kuwapigia kura viongozi wanaowapenda kama ilivyo kwenye mataifa mengine duniani, ukiwemo uchaguzi wa urais mwaka 2026.

Mfumo wa raia wa Somalia kuwachagua viongozi wao kwa kuwapigia kura, ulifutwa baada ya dikteta Siad Barre mwaka 1969 na baada ya kuanguka kwa utawala wake 1991, na mfumo wa kisiasa nchini Somalia kuhamia kwa wakuu wa koo mbalimbali kufanya maamuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *