Zari: natamani kumuona Zuchu ‘Young, Famous & African’ , Tanasha hafai

Dar es Salaam. Mzazi mwenzie na Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari the Boss Lady’ amedai  kinachokwamisha Wabongo wengi kutoshiriki kwenye kipindi cha ‘Young, Famous & African’ ni umbea.

“Wabongo wanapenda umbea sana hiyo ni sehemu ya utamaduni wa Kitanzania. Sidhani kama umbea utaweza kufanya kazi kwenye Young, Famous & African,” alisema Zari, huku akiweka wazi kipindi hicho kinazingatia drama ya uhalisia wa maisha.

Hata hivyo, amesema anatamani  kumuona mwanamuziki Zuchu, akishiriki kwenye kipindi hicho.

“Hebu tumweke Zuchu kwenye kipindi, akiwa pale ndio ataelewa kwanini Diamond alisema yeye ni msanii wake,” amesema Zari.

Aidha kwa upande wa Tanasha Donna ambaye pia amezaa na Diamond, Zari amesema licha ya urembo wake lakini hafai kwenye kipindi hicho kutokana na upole alionao. Huku akitamani kumuona Vera Sidika kwenye shoo hiyo.

“Hakuna vigezo maalumu; Netflix ndiyo wanaamua nani aingie kwenye kipindi,” amesema Zari.

Ikumbukwe ‘Young, Famous & African’ ilianza kuoneshwa kwa mara ya kwanza Machi 18, 2022.