Zambia yatangaza maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha rais mstaafu Lungu

Zambia imetangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa Jumamosi, Juni 7, 2025, kufuatia kifo cha aliyekuwa rais Edgar Lungu, aliyefariki siku ya Alhamisi, Juni 5, 2025, nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 68, serikali imetangaza.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Edgar Lungu, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 68, aliongoza nchi hiyo kubwa lakini yenye wakazi wachache kusini mwa Afrika (takriban watu milioni 19) kuanzia mwezi Januari 2015 hadi mwezi Agosti 2021, aliposhindwa katika uchaguzi wa urais dhidi ya kiongozi wa sasa Hakainde Hichilema.

“Serikali ya Jamhuri ya Zambia inapenda kufahamisha umma kwamba rais Hakainde Hichilema ameidhinisha mazishi ya kitaifa ya rais wa sita Edgar Lungu, aliyefariki Juni 5,” mkurugenzi katika ofisi ya rais Patrick Kangwa amesema.

Serikali imesema bendera zitapeperushwa nusu mlingoti kuanzia Jumapili hadi Jumamosi, na hafla za burudani zitasitishwa katika kipindi hiki.

Bw. Kangwa amesema mwili wa rais huyo wa zamani utawasili nchini Zambia siku ya Jumatano, na kwamba Hoteli ya Belvedere Lodge katika mji mkuu, Lusaka, imechaguliwa kuwa mahali atazikwa.

Bw. Lungu alikuwa akipata matibabu maalum katika kliniki moja mjini Pretoria, kulingana na chama chake cha kisiasa, Patriotic Front.

Amekuwa akiugua achalasia ya mara kwa mara, hali ya mishipa ya fahamu ya umio, ambayo hapo awali alitibiwa huko Afrika Kusini.

Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Amnesty International, utwala wa Bw. Lungu uliifikisha Zambia kwenye ukingo wa kuporomoka, na “ukandamizaji mkali dhidi ya haki za binadamu” na “mashambulio ya kinyama dhidi ya aina zote za upinzani.”

Kwa upande wa kijamii, alikuwa mhafidhina, akiamini, kwa mfano, kwamba haki za wapenzi wa jinsia moja (LGBT+) zilikuwa dhana ya “kigeni”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *