
Tasila Lungu, mbunge wa eneo la Chawama katika mji mkuu Lusaka, anashikiliwa na idara ya usalama baada ya kurejea nchini kutoka Marekani, Tume ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DEC) imesema. Anatuhumiwa kwa “kumiliki mali inayoshukiwa kuwa mapato ya uhalifu na utakatishaji fedha,” msemaji wa DEC Allan Tamba amewaambia waandishi wa habari.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
DEC imetaja shamba lenye thamani ya kwacha milioni 8.8 (kama dola 316,000) ambalo Tasila Lungu, 41, alikuwa akimiliki mashariki mwa Zambia kuanzia Januari 2015 hadi Desemba 2022. Binti ya Edgar Lungu, ambaye alitawala Zambia kati ya mwaka 2015 na 2021, alikamatwa hapo awali mwezi Mei 2024 pamoja na mama yake na dada yake. Familia ilikuwa imeshutumu wakati huo “sababu za kisiasa”. Kaka yake, Dalitso, pia anatuhumiwa kwa ufisadi.
Mnamo mwaka 2023, polisi walivamia nyumba ya familia hiyo, wakimtuhumu mke wa rais wa zamani kwa kuiba magari. Bw Lungu alijiuzulu kama rais wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika yenye utajiri wa shaba mwaka 2021 baada ya mkongwe wa upinzani Hakainde Hichilema kushinda uchaguzi wa kishindo. Alitangaza kuwa anapanga kugombea tena urais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka ujao.