Zaidi ya watu Milioni saba wanakabiliwa na baa la njaa nchini Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa unasema watu Milioni 7.7 nchini Sudan Kusini, wanakabiliwa na baa la njaa, wengi wakiwa ni wakaazi wa eneo la Kaskazini Mashariki, lililokabiliwa na machafuko hivi karibuni.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Shirika la mpango wa chakula WFP linasema, hali ni mbaya na mamilioni ya watu nchini Sudan Kusini, wanahitaji msaada wa haraka.

Waakazi wa jimbi la Upper Nile ndio walioathiriwa zaidi, hali ambayo imechochewa na mapigano ya hivi karibuni kati ya waasi wa White Army na jeshi la serikali na kukwamisha shughuli za kila siku za kiuchumi.

Mbali na uhaba wa chakula, wakaazi wa Upper Nile hawana makaazi. Kabla ya kuanza kwa vita, watu hao walikuwa wanategemea vyakula kutoka Ethiopia, lakini kwa sasa wamekimbia kwa kuhofia maisha yao.

Majimbo mengine sita, yapo katika hali mbaya, huku wakimbizi wapatao Milioni 1.1 waliokimbilia Sudan Kusini kutoka Sudan, pia wakihitaji chakula na misaada nyingine ya kibinadamu.

Mbali na baa la njaa, Sudan Kusini pia inakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umesababisha vifo vya watu 700 na wengine zaidia ya 40,000 kuambikizwa tangu mwezi Septemba mwaka uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *