
Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya raia 542 wameuawa eneo la kaskazini mwa jimbo la Darfur nchini Sudan, kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita, na kuonya kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa Volker Turk mkuu wa afisi ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, vita vinavyondelea nchini Sudan havina mipaka na mapambano ya vikosi vya serikali na wale RSF yanazidi kusababisha maafa.
Turk sasa anataka kila juhudi kufanyika kuwalinda raia wakati huu wapiganaji wa RSF wakionya kuhusu mapigano makali dhidi ya vikosi vya serikali na washirika wao hasa katika jiji la Al Fasher, Turk pia ameelezea wasiwasi wake kuhusu kanda ya vídeo inayosambaa kwenye mitandao ikionesha namna watu wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa RSF walivyowaua wanaume zaidi ya 30.
Jimbo la Darfur limekuwa uwanja wa mapambo tangu vita kuanza miaka miwili iliopita, kila pande ikilienga kudhibiti jimbo hilo.
Vita nchini Sudan vimesababisha maelfu ya raia kufariki na wengine kukimbia makwao, kwa kile mashirika ya kiraia yamesema Sudan imeandikisha idadi kubwa ya watu waliokimbia makwao kutoka na vita.