Zaidi ya watu 13 wameuawa katika shambulio la kujitolea mhanga

Ziadi ya watu 13 wameuawa baada ya mlipuaji wa kujitolea mhanga kulenga shughuli ya kuwasajili kurutu wa jeshi nchini Somalia.

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Kwa mjibu wa taarifa ya wizara habari, tukio hilo lilitokea katika kambi ya Xero Damaayo Kusini mwa jiji la Mogadishu, mlipuaji huyo akilenga vijana waliokuwa wakisajiliwa kujiunga na jeshi, japo hakuna aliyekiri kuhusika na shambulio hilo.

Ni kisa kinachojiri siku moja tu baada ya siku ya Jumamosi Kanali, Abdirahmaan Hujaale kuuawa na wapiganaji wanaodaiwa kuwa wa kundi la Kigaidi la al-Shabab, ambao sasa wanakisiwa kwamba wamejiunga bila kufahamika kwaserikali na vyombo vya usalama.

Tukio kama hili pia liliwahi kuripotiwa mwaka 2023 ambapo zaidi ya wanajeshi 25 waliuawa.

Kundi la magaidi wa al shabab likitekeleza mashambulio kwenye kambi za jeshi nchini Somalia na majengo ya serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *