Israel usiku wa kuamkia leo imetekeleza mashambulio mfululizo ya anga kwenye eneo la Gaza, ambapo watu zaidi ya 100 wameripotiwa kuuawa na wengine mamia kujeruhiwa, haya yakiwa ni mashambulio ya kwanza makubwa tangu kumalizika kwa muda wa makubaliano ya kusitisha mapigano na kundi la Hamas.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Ofisi ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu imesema mashambulizi hayo yameamrishwa kufanyika baada ya Hamas kukataa kuwaachia mateka wa Israel pia kukata mapendekezo ya amani yaliyowakilishwa na mjumbe wa Marekani Steve Witkoff na wapatanishi wengine kwenye mzozo huo wa Gaza.
Hamas kwa upande wake imemlaumu Netanyahu kwa kile wanasema ni kufuta makubaliano kwenye mpango wa amani wa awamu ya Kwanza, hali wanaosema itahatarisha maisha ya mateka walioko Gaza.
Siku ya Jumatatu ,mjumbe wa Marekani Witkoff alikuwa ametoa pendekezo la kuachiwa kwa mateka watano wa Israel walio hai ambao wangebadilishwa na idade kubwa ya wafungwa wa Palestina wanaouziliwa kwenye magereza ya Israel, mpango ambao hata hivyo hamas haikuuukubali.