
Umoja wa Mataifa umesema vurugu zilizoibuka mashariki mwa Kongo zimewalazimu katika kipindi cha mwezi mmoja, watu 100,000 kutoroka makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema idadi kubwa ya watu hao wanaishi katika mazingira duni kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili wake.
Wengi wa watu 100,000 waliokimbia makazi yao nchini Uganda na Burundi wanajikuta katika “hali mbaya.”
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, zaidi ya watu 100,000 waliokimbia vita mashariki mwa DRC wamepata hifadhi katika muda wa chini ya miezi mitatu katika nchi jirani za Uganda na Burundi. Mapigano katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini yamewalazimu watu kutoroka makazi yao. Lakini hali yao inaleta matatizo mengi katika nchi zinazowapokea, kama ilivyoelezwa na msemaji wa UNHCR mjini Geneva, Eujin Byun.
Hali katika nchi jirani ni mbaya, kwanza kwa sababu nchi hizi mbili tayari zimepokea mamilioni ya wakimbizi. Kwa hiyo tunaweza kuona mzigo mzito walio nao katika kuwahifadhi na kuwakaokea wakimbizi hawa. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa fedha wa hivi majuzi na uhaba wa fedha, hatuwezi kukabiliana mara moja na dharura hii. Hii ina maana kwamba idadi kubwa ya wakimbizi wanaowasili kutokana na mzozo nchini DRC wanajikuta katika hali ya msongamano mkubwa wa maisha, na ukosefu wa huduma za msingi kama vile maji, chakula na malazi. Aidha, kwa sasa tumebaini wagonjwa wanane wa kipindupindu, jambo linaloonyesha kuwa mfumo wa afya hautoshi katika nchi hizi mbili, hivyo kuongeza hatari ya kuenea kwa magonjwa mengine.