
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Tianjin, Kaskazini mwa China, wanasema kuwa wanaume ambao wanaokunywa sharubati ya zabibu mara tano kwa siku au hata zaidi kwa wiki, wanaweza kupunguza tatizo la kukosa hamu wakati wa tendo la ndoa.
Sampuli ya wanaume 300 wenye tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume walihusishwa sambamba na wengine 300 ambao wako ‘fit’ kwa gwaride la kitandani.
Ilibainika kuwa wale waliokunywa sharubati ya zabibu kwa zaidi ya mara tano, waliimarisha weledi wao wa kupiga kwata chumbani tofauti na ilivyokuwa kwa siku za nyuma.
Ukosefu wa nguvu za kiume ni tatizo ambalo huwakumba sana wanaume wazee hasa wenye umri wa miaka 60 na zaidi.
Uzoefu unaonyesha baadhi ya magonjwa kama vile matatizo ya moyo, bawasiri ba mengneyo mbalimbali husababisha wanaume wengi kukosa nguvu za kiume.
“Sharubati ya zabibu haina kemikali hatari na ina madini ambayo yana manufaa kiafya. Ile ya zabibu nyekundu ni nzuri zaidi kwa sababu ina kemikali ambazo zinazuia seli muhimu kuharibiwa,” inasema sehemu ya utafiti huo uliofanywa na kikosi cha wataalamu na watafiti wakiongozwa na mtafiti mkuu, Liwei Wua ulieleza.
Watafiti hao pia walichunguza umuhimu wa sharubati ya nyanya, matunda, machungwa, limau na paipai lakini ile ya zabibu ndiyo ilipatikana kuwa na manufaa kwa waliopungukiwa na hamu ya kufanya mapenzi.
Aidha, watafiti pia walichunguza maziwa na aina mbalimbali za soda, lakini bado wakapata sharubati ya zabibu kama kichocheo muhimu kinachowasaidia wanaume wazee kuongeza ashki.
Utafiti huo pia ulibaini kuwa sharubati nyekundu ya zabibu, husaidia kuepesha magonjwa ya moyo kwa kuimarisha usambazaji wa damu mwilini kwa kuzuia mishipa kuzibwa na mafuta.