Yuji Iwasawa ateuliwa kuwa mkuu mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), chombo cha juu cha mahakama cha Umoja wa Mataifa, siku ya Jumatatu imemteua Mjapani Yuji Iwasawa kama mkuu wake mpya, akichukua nafasi ya Nawaf Salam, waziri mkuu mpya wa Lebanoni.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Yuji Iwasawa anamrithi Nawaf Salam, Waziri Mkuu mpya wa Lebanoni. Yuji Iwasawa atachukua nafasi ya mkuu wa mahakama ya Hague hadi muda wa Nawaf Salam utakapokamilika tarehe 5 Februari 2027.

Mjapani huyo mwenye umri wa miaka zaidi ya 70 atahudumu kama mkuu wa ICJ hadi muda wa Bw Salam utakapokamilika mnamo Februari 5, 2027, mahakama hiyo iliyoko Hague, imesema katika taarifa.

Rais Iwasawa amekuwa mjumbe wa ICJ tangu mwezi Juni 2018. Hapo awali, alikuwa profesa wa sheria za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Tokyo na aliwahi kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.

Migogoro kati ya mataifa

ICJ, iliyoundwa mnamo mwaka 1946, inasuluhisha mizozo kati ya mataifa. Wakati mwingine inafananishwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ambayo pia ina makao yake mjini THague na kuwahukumu watu wanaoshukiwa kwa uhalifu mbaya zaidi kufanywa duniani kama vile uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

ICJ kwa sasa inashughulikia kesi kadhaa zenye hadhi ya juu.

Kesi za wasifu wa juu

Inaangalia hasa malalamiko yaliyowasilishwa na Afrika Kusini kwamba Israel inafanya mauaji ya halaiki katika mashambulizi yake dhidi ya Ukanda wa Gaza.

ICJ pia inajadili kesi kati ya Ukraine na Urusi kuhusu vamizi wa Februari 2022.

Na mahakama hii inatayarisha maoni ya ushauri juu ya wajibu wa nchi katika masuala ya mabadiliko ya Tabainchi.

Jukumu la kiitifaki

Mkuu anaongoza jopo la majaji 15 lakini ana jukumu kubwa la kiitifaki, akitoa hotuba kwa niaba ya mahakama na kuwakilisha taasisi kote ulimwenguni. Pia anasoma maamuzi ya ICJ.

Lakini sauti ya mkuu wa mahakama ina uzito sawa na ile ya majaji wengine katika maamuzi ya kimahakama, isipokuwa katika kesi ya usawa wa kura, ambapo kurayake ni ya maamuzi.