Yemen yatishia kuifungia tena Israel Bahari Nyekundu

Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen limeonya kuwa litarejea kwenye operesheni zake za kijeshi za majini za kuifungia Israel Bahari Nyekundu (Bahari ya Sham) kama Tel Aviv itashindwa kuheshimu muda iliopewa wa kukomesha mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Ukanda wa Ghaza.