Yemen yaitwanga meli ya kivita ya Marekani kwa mara ya saba

Msemaji wa Jeshi la Yemen ametangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanya operesheni nne za kijeshi dhidi ya utawala wa Kizayuni na Marekani, muhimu zaidi ikiwa ni kuishambulia manuwari ya kubebea ndege ya Marekani iitwayo “Truman” kaskazini mwa Bahari Nyekundu.