Yemen yaangusha ndege ya 15 ya  kisasa ya kijasusi ya Marekani

Jeshi la Yemen limetangaza kuangusha kwa mafanikio ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper baada ya kuingia katika anga ya nchi hiyo kinyume cha sheria na kufanya operesheni za kijeshi katika mkoa wa magharibi wa al-Hudaydah.