Yemen: Idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya Marekani kwenye bandari yaongezeka hadi 58

Waasi wa Houthi wa Yemen wameripoti idadi mpya ya vifo vya watu 58 siku ya Ijumaa, Aprili 18, katika shambulio la Marekani kwenye bandari ya mafuta, shambulio baya zaidi tangu kuongezeka kwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Idadi ya waliouawa kutokana na shambulio la adui, Marekani, kwenye vituo vya Ras Issa imeongezeka hadi 58 na watu 126 waliojeruhiwa,” idhaa ya waasi ya Al-Massirah imesema, ikitoa ikinukuu mamlaka za ndani huko Hodeida. Ripoti ya awali ilitaja watu 38 waliouawa na 102 kujeruhiwa.

Mashambulio hayo ni mojawapo ya yale yaliyosababisha idadi kubwa zaidi ya vifo vya watu nchini Yemen, tangu Rais Donald Trump alipoanzisha kampeni ya kijeshi dhidi ya kundi la Wahouthi.

Kwenye taarifa yake, Jeshi la Marekani limesema vikosi vyake vimechukua hatua ya kusambaratisha chanzo cha mafuta kinachotumiwa na waasi wa Houthi. Limesema mashambulizi  hayo yatawanyima waasi hao mapato yaliyowezesha kufadhili shughuli za waasi wa Houthi kwa zaidi ya miaka 10.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *