
YANGA imeanza mapema harakati za kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao huku ikipiga hodi katika Ligi Kuu Kenya kwenye kikosi cha Kenya Police FC.
Yanga ambayo hadi sasa imetajwa kuwa katika harakati za kumsajili Jonathan Sowah kutoka Singida Black Stars na Jibril Sillah wa Azam FC, pia imeonekana kuvutiwa na kiungo mshambuliaji Mohammed Omar Ali Bajaber.
Kiungo huyo raia wa Kenya mwenye uwezo wa kushambulia kutokea kulia na kushoto, pia anacheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu Harambee Stars.
Taarifa kutoka Kenya zinabainisha kuwa, mabosi wa Yanga wana uhitaji mkubwa na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 na kama mambo yatakwenda vizuri huenda wakamalizana naye hivi karibuni kwani inaelezwa wakati wowote atakuja Tanzania kwa ajili ya suala hilo.
Hesabu za mabosi wa Yanga sambamba na benchi la ufundi chini ya Kocha Miloud Hamdi ni kutaka kuongeza mtu wa maana kabla ya kufanya uamuzi wa kumuuza Stephane Aziz Ki ambaye anatajwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Kocha wa zamani wa Kenya Police, Francis Baraza raia wa Kenya, ameliambia Mwanaspoti kuwa anazo taarifa za mchezaji huyo kutakiwa na Yanga kutokana na kuanza kuripotiwa kwa kasi nchini kwao.
“Ni taarifa ambazo zinazungumzwa sana huku kuwa kiungo huyo anafanya mazungumzo na moja ya timu Tanzania kwaajili ya kujiunga nayo msimu ujao,” alisema Baraza ambaye kwa sasa anaifundisha Kakamega Home Boys inayoshika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Kenya.
Akizungumzia ubora wa Bajaber, Baraza alisema ni mchezaji mzuri mwenye uwezo wa kucheza winga zote mbili kulia na kushoto lakini pia ni kiungo mzuri wa kushambulia.
“Bajaber ni kiungo mzuri, endapo Yanga wat