Yanga yafuzu kibabe 32 bora Shirikisho ikiipa mkono Copco

Dar es Salaam. Yanga imewafuta machozi mashabiki wake ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Copco ya Mwanza leo Januari 26, 2025 katika Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam katika Kombe la Shirikisho la CRDB.

 Nyingine ni Stand United, Biashara United, Mbeya Kwanza, Transit Camp, Town Star, Polisi Tanzania, Songea United, Kiluvya, JKT Tanzania, Leo Tena na Kagera Sugar.

Pia kuna Tabora United, Cosmopolitan, Bigman, Giraffe Academy, Geita Gold, Namungo, Coastal Union, Azam, Fountain Gate, Tanzania Prisons, Pamba Jiji, KMC, Mashujaa, Singida Black Stars, Mambali Ushirikiano, Mtibwa Sugar, TMA Stars, Green Warriors na Mbeya City.

Kikosi cha Yanga leo kiliundwa na Aboutwalib Mshery, Israel Mwenda, Nickson Kibabage, Jonas Mkude, Bakari Mwamnyeto, Salum Abubakar/John Misheto, Shekhan Khamis/Dickson Job, Duke Abuya, Prince Dube/Maxi Nzengeli, Aziz Ki/Kibwana Shomari na Farid Mussa/Mudathir Yahya.

Copco kikosi chao kilikuwa na Joseph Adam, Berkhhof Ahab William, Mohamed January Alex, Andrew Frank Mahende, Yusuph Amos Mgeta, Ally Athuman Ekwabi, Simon Bulemo Bazili/Dickson Charles Mwizarubi, Rajab Rashid Rajab/Ibrahim Hashim Njohole, Rajesh Biku Kotecha/John Elias Masanzu, Joseph Moshi Samson/Bahati Posso na Jagadi Sola Gushaha/ Said Juma Manoni.

Mabao ya Yanga katika mechi ya leo yalifungwa na Shekhan Ibrahim, Prince Dube, Maxi Nzengeli, Duke Abuya na Mudathir Yahya.

Shekhan Ibrahim alikuwa wa kwanza kuifungia Yanga bao katika mechi ya leo akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona wa Farid Musa.

Bao hilo lilidumu hadi filimbi ya mapumziko ilipopulizwa.

Kipindi cha pili kilikuwa cha neema zaidi kwa Yanga kwani ilipata mabao manne ambayo yalitanguliwa na bao la Dube katika dakika ya 58 akiunganisha pasi ya Israel Mwenda.

Yanga ilipata bao la tatu katika dakika ya 68 kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Maxi Nzengeli katika dakika ya 68.

Dakika ya 78, Duke Abuya alifunga bao la nne la Yanga akiunganisha krosi ya Nickson Kibabage na ushindi wa Yanga ulihitimishwa na bao la Mudathir Yahya katika dakika ya 84 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Israel Mwenda.

Kwa ushindi huo, Yanga inakuwa timu ya 31 kufuzu hatua ya 32 bora.