
Yanga imewasili ikiwa imekamilika kwenye kikao maalumu cha Waziri Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Palamagamba Kabudi, huku wakitenganishwa na viongozi wa Simba.
Kikao hiki ni maalumu kwa ajili ya kujadili mustakabali wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo ambao uliahirishwa siku ya mechi, baada ya Simba kulalamika kuwa walizuiwa na watu waliowataja kama walinzi wa Yanga kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam sehemu ambayo mchezo huo ulitarajiwa kufanyika, Machi 8.
Kikao hicho ambacho kinaendelea kwenye Ofisi za Wizara zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga imekuja ikiwa imekamilika ikiongozwa na rais wa klabu hiyo injinia Hersi Said na makamu wake Arafat Haji.
Mbali na viongozi hao wawili wa juu, pia wamo wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Yanga Makaga, Gerald Kihinga, Alexander Ngai, Munir Said, Seif Gulamali na Rodgers Gumbo na Afisa Mtendaji Mkuu Andre Mtine aliyefika sambamba na mwanasheria wa klabu hiyo ambaye anatoka kwenye kampuni moja ya sheria hapa nchini.
Viongozi hao waliwasili kwa makundi tofauti uwanjani hapa ambapo kiongozi wa kwanza kufika alikuwa rais wa Shrikisho la Soka Tanzania Wallace Karia ambaye alifuatiwa na viongozi wa wizara wakiongozwa na Katibu Mkuu Greyson Msigwa, Waziri Kabudi na naibu wake Hamis Mwinjuma maarufu kwa jina Mwana FA.
Simba,Yanga watenganishwa
Kwenye kikao hicho viongozi wa Simba na Yanga wametanganishwa ambapo kilianza kikao ambacho kiliwahushisha wale wa Yanga peke yao na baada ya kumalizika ndiyo viongozi wa Simba wataruhusiwa kuingia.
Yanga imeingia kwenye kikao hicho kuanzia saa 4:00 asubuhi baada ya wajumbe wake wote kukamilika ambapo uongozi kamili wa klabu hiyo upo hapa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam tayari kwa kuitikia wito huo.
Hata hivyo, kikao hicho kitafanyika kwa Waziri Kabudi kuwasikiliza kwanza Yanga, ambapo baadaye atahamia kwa kundi lingine ambalo litaongozwa na viongozi wa Simba.
Taarifa kutoka ndani ya wizara ni kwamba baada ya kikao cha Yanga kukamilika kitafuatia kikao Cha Waziri Kabudi na uongozi wa klabu ya Simba.
Kikao Cha Simba na Waziri kimepangwa kuanza saa nane mchana.
Inaelezwa kwamba serikali imeamua kuwatenganisha mabosi wa klabu hizo kongwe nchini kuhofia mvutano mkubwa endapo wangekutana kwa pamoja.
Mbali na viongozi wa Simba na Yanga, pia mabosi wa juu wa Bodi ya Ligi Tanzania TPLB wakiwemo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Steven Mnguto na Afisa Mtendaji Mkuu Almas Kasongo