
Wakati Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mumewe Francis Ciza ‘Majizo’ leo wakifurahia miaka mitatu ya ndoa yao, iliyofungwa siku kama ya leo mwaka 2021, msanii na mfanyabiashara Hamisa Mobetto naye anaanza rasmi maisha ya ndoa baada ya kuoana na Stephen Aziz Ki.
Nyota hawa wanne Majizo, Lulu, Aziz Ki na Hamisa Mobetto wote wamefunga ndoa siku inayofanana kasoro miaka.
Majizo na Lulu walifunga ndoa siku ya Jumanne Februari 16, 2021, katika Kanisa la St Gasper lililopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, naye nyota wa soka Stephane Aziz Ki na mkewe Hamisa wamefunga leo Februari 16, 2025 katika moja ya msikiti uliopo Mbweni jijini Dar es Salaam.
Hamisa ameolewa kwa mahari ya ng’ombe 30 na kiasi cha pesa Sh30 milioni na hii itakuwa ndoa ya kwanza kwa msanii huyo.
Wapendanao hawa wanne wanaenda kuchangia siku muhimu kwenye maisha yao, ambayo ni kumbukumbu ya ndoa zao.
Mbali na kumbukumbu za ndoa hizo utakumbuka Hamisa na Majizo ambaye ni mume wa Lulu wamebahatika kupata mtoto wa kike aitwaye Fantasy.
Huku kwa upande wa Lulu tayari ana watoto wawili na Majizo, ambao ni wakike.