Yanayoendelea viwanja vya Leaders Club kwenye msiba wa King Kikii

Dar es Salaam, Mwili wa msanii mkongwa wa muziki wa dansi nchini Boniface Kikumbi maarufu ‘King Kikii’ tayari umewasili katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kupewa heshima za mwisho.

King Kikii ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 15,2024, nyumbani kwake Mtoni Kwa Aziz Ally jijini Dar es Salaam kwa ugonjwa wa saratani ya ini. Mwili wake unaagwa leo Novemba 18,2024 katika viwanja hivyo na kisha kupumzishwa kwenye makaburi ya Kinondoni.

Ratiba ya msiba

Saa 5 mpaka saa 6 mchana

Mwili wa marehemu utapelekwa
kuelekea Leaders

Saa 6 mpaka saa 8 mchana

Ibada na kuaga mwili
Saa 8:00 mpaka saa 8:20 mchana

Wasifu wa marehemu
Saa 8:20 mpaka saa 9.30 mchana
Salamu za rambirambi

Saa 9:30 mpaka saa 10 mchana

Msafara kuelekea makaburini kwa ajili ya
ya maziko

Saa 10 jioni
Mazishi makaburini Kinondoni

King Kikii alizaliwa mwaka 1947, enzi za uhai wake alitamba na vibao vingi ikiwemo kile maarufu cha ‘Kitamaa Cheupe’.