Yamkini Facebook ikatozwa faini ya dola bilioni 2 ikipatikana na hatia ya kuchochea vita

Mahakama Kuu ya Kenya imetoa uamuzi kwamba kampuni ya Marekani ya Meta, inayomiliki Facebook, inaweza kushtakiwa nchini humo kwa tuhuma za kuchochea chuki iliyopelekea vita vya kikabila nchini Ethiopia. Kesi hiyo, inayodai fidia ya dola bilioni 2.4, (takriban shilingi trilioni 3 za Kenya kwa makadirio ya sasa) imewasilishwa na watafiti wa Ethiopia na wanaharakati wa haki za binadamu wa Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *